Alejandro Kuropatwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alejandro Kuropatwa (Oktoba 22 1956 - Februari 5, 2003) alikuwa mpiga picha wa Argentina.

Alizaliwa katika familia ya wahamiaji wa Kiyahudi katika mji wa Buenos Aires, katika ya mwaka 1979 na 1982 alijifunza upigaji picha katika chuo cha Fashion Institute of Technology kilichopo katika jiji la New York na kisha alirudi katika mji wa Buenos Aires ambapo aliendeleza taaluma yake ya upigaji picha.

Alikuja kuwa maarufu zaidi kwa sababu ya picha zake za watu maarufu na wasanii wa Argentina kama Charly Garcia, Gustavo Cerati na Fito Páez, Kuropatwa aligundulika kuwa na virusi vya Ukimwi mwaka 1984 na mwaka 2002 alishinda tuzo ya Konex Award kama mpiga picha mwenye mvuto zaidi nchini Argentina.[1]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Kuropatwa alifariki mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 47.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Alejandro Kuropatwa" (kwa Kihispania). Fundación Konex. Iliwekwa mnamo 2008-04-20. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alejandro Kuropatwa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.