Aina za udongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Aina za Udongo

Aina za udongo hutofautishwa kutokana na tabia za udongo na mahitaji ya binadamu katika kuutumia.

Udongo ni mchanganyiko wa vipande vidogo vya mwamba na madini vilivyosagwa pamoja na mata ogania hasa kwenye tabaka la juu.

Aina za udongo zinaweza kutofautishwa kutokana na tabia za kifizikia na tabia za kikemia.

Ukubwa wa vipande ndani ya udongo ni muhimu, pia kiasi gani ni imara au la, halafu kemikali au kampaundi gani zinapatikana ndani yake.

Tabia hizo zote zinasababisha tofauti kubwa katika matumizi ya udongo kama ardhi ya shamba, ardhi ya kujengewa kwa majengo au malighafi kwa vifaa vinavyotumiwa na binadamu.

Aina za udongo[hariri | hariri chanzo]

  • Udongo kinamo au udongo wa mfinyanzi - Udongo wa aina hiyo ni udongo ambao una chembechembe ndogo sana na una tabia ya kushikamana, pia udongo hupenyeza maji ardhini kwa haraka na hivyo husababisha maji kutuama kwa muda mrefu.
  • Udongo tifutifu - Aina hii ya udongo kwa asilimia kubwa ndiyo aina ya udongo ambao una rutuba na unafaa kwa kilimo kwani una chembechembe ndogo ambazo huruhusu ustawi wa uoto wa asili pamoja na mazao vizuri na kwa urahisi kwa sababu hupitisha maji kwa urahisi.
  • Udongo wa kichanga - Ni udongo wenye chembechembe kubwa na hivyo huruhusu maji kupita kwa haraka sana. Kutokana na hali hiyo udongo huu haufai sana kwa kilimo cha mazao kwani haukai na unyevunyevu.

Sifa za udongo[hariri | hariri chanzo]

Udongo una sifa zifuatazo:

  • Rangi ya udongo hutuwezesha kujua aina za kemikali zilizomo. Kwa mfano udongo mwekundu una madini ya chuma lakini udongo wa kijivu hauna madini ya chuma.
  • Unamu wa udongo ni ukubwa wa chembechembe za udongo. Udongo wa kichanga una chembechembe kubwa, udongo wa tifutifu una chembechembe ndogo na udongo wa mfinyanzi una chembechembe ndogo zaidi.
  • Muundo wa udongo ni uwezo wa udongo kushikamana au kutoshikamana. Kwa mfano udongo wa mfinyanzi hushikamana lakini udongo wa kichanga haushikamani.
  • Upenyeza wa udongo ni uwazi kati ya chembe na chembe ambao huwezesha maji kupenyeza.
  • Rutuba ni uwezo wa udongo kulisha mimea. Hutegemea mboji iliyomo katika udongo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]