Udongo kinamo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Udongo wa kinamu nchini Estonia

Udongo kinamo (udongo wa kinamu, pia udongo wa mfinyanzi, ing. clay) ni aina ya udongo ambao una chembechembe ndogo sana na una tabia ya kushikamana.

Udongo wa aina hii huwa na uwezo mkubwa wa kushika maji ndani yake. Ganda la udongo kinyamo, tofauti na mchanga, haupitiki kirahisi na maji.

Udongo kinamo huwa mgumu ukikauka kabisa. Tangu miake mielfu ulitumiwa na binadamu kwa kufinyanga vyombo. Maana udongo huu ukiwa katika hali bichi unakubali umbo lolote linalopewa na mfinyanzi. Kama unachomwa, yaani kuokwa katika tanuri kwa joto la sentigredi 1000 au zaidi, tabia yake inabadilika. Huwa mgumu, na haubadilishwi tena na maji. Vitu kama matofali ya ujenzi na vyombo kama sahani, vyungu au sufuria hutengenezwa kwa njia hii ambavyo vinaweza kudumu miaka mingi visipovunjwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Kujisoemea[hariri | hariri chanzo]