Ahmad Basheikh Husein

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ahmad Basheikh Husein
Jina la kuzaliwa Ahmad Basheikh Husein
Alizaliwa 1909
Alikufa 11 Desemba 1961
Nchi Kenya, Mombasa
Kazi yake Mshairi

Ahmad Basheikh Husein (Mombasa, 1909 - Mombasa, 11 Desemba 1961) alikuwa mshairi na mwandishi katika usultani wa Mombasa. Aliandika ushairi na hadithi zake kwa Kiswahili. Aliandika vitabu vyake kwa sultani wa Mombasa.

Alikuwa mwana wa Husein na Bibi wa Mwinyi Matano. Alikuwa mjomba wa mshairi Ahmad Nassir Juma.

Ahmad Nassir Juma aliandika mistari na mashairi ya Ahmad Basheikh Husein.

Alijulikana kuandika mashairi mengi kama Kunena nawe sikomi, Mbasi, Wanawake, Ila kafati shuarai au Tumi Nakutuma.

Mashairi yake[hariri | hariri chanzo]

 • Kunena nawe sikomi
 • Mbasi
 • Wanawake
 • Ila kafati shuarai
 • Tumi Nakutuma
 • Mahaba Matungu
 • Mahaba si tamu
 • Wake kwa waume
 • Usia kwa mke mwana
 • Asiyetaka kufunzwa
 • Taa yetu ya thureya imezimika ghafula kifo cha Mbarak Ali Hinawi
 • Mimi sina neno huba zimekwisha

Mistari ya Mimi sina neno huba zimekwisha[hariri | hariri chanzo]

Lipi kuu mno ~ la kunionesha.

Ni mangi maneno ~ na kuhakikisha

Mimi sina neno ~ huba zimekwisha.

Hiyo siyo ndiya ~ ya kuridhi moyo

Watu wakutaya ~ kwa uyafanyayo

Walaje pamoya ~ na mume mwenziyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • Knappert, J. (1982). Four Centuries of Swahili Verse.
 • Frankl, P. J. (1991). Mombasa under the BuSaʿidi A Leaf from the Taylor Papers (SOAS MS 47757, folio 50). Zeitschrift der Deutschen Morgenländischen Gesellschaft, 141(1), 131-138.
Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ahmad Basheikh Husein kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.