Aga Khan Academy, Mombasa
Aga Khan Academy, mjini Mombasa ni moja kati ya shule za Aga Khan Academy, zinaozfunza elimu ya kiwango cha kimataifa na iliyo bora katika aina yoyote ya elimu.
Shule hii hutoa elimu pana yenye masomo mengi, na husisitiza masomo ya sanaa. Wanafunzi hujifunza masomo mbalimbali ikiwemo, historia; fasihi; masomo ya sayansi kama fizikia, baiolojia na kemia; falsafa na maadili; ujuzi wa lugha ya kigeni na somo la tamaduni za kigeni; somo la dini; historia, nadharia na ukosoaji wa sanaa na sayansi ya kijamii, pamoja na sayansi ya siasa, serikali na uchumi wa kimataifa.
Kujiunga na shule hii hutegemea mafanikio ya mwanafunzi. Pia ni kwa njia-kipofu - ambayo ni, uteuzi hautegemei uwezo wa kulipa karo lakini kwa usahihi wa vigezo anuwai, kama vile uwezo wa mwanafunzi kufaulu mtihani.
Mfumo wa elimu
[hariri | hariri chanzo]Shule ya Aga Khan Academy, Mombasa ni inatekeleza mfumo wa elimu inayojulikana kote duniani inayoitwa International Baccalaureate kwa Shule ya Msingi. Mfumo huu unafaa kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 5-11 katika madarasa 1-6, inayolenga katika maendeleo ya mtoto, kwa kushughulikia maswala ya kijamii, kimwili, na mahitaji ya kitamaduni na kimaadili, na vilevile kuwapa wanafunzi msingi imara katika maeneo muhimu ya elimu. Mnamo Januari 2005, Aga Khan Academy (Shule ya msingi - madarasa ya chini), ilituzwa "Candidate School" kutoka kwa cham cha International Baccalaureate Organization (IBO).
Wanafunzi walio katika Darasa za Kati, kwa umri 11-16, ni hutumbukizwa kwenye mazingira yenye changamoto ambayo husisitiza ustadi na ujuzi wa kazi za kawaida, uwezo wa kuchambua na kufikiri, uwezo wa kujitegemea na nidhamu ya kazi nzuri, na masomo ya kompyuta na ustadi katika ujuzi wa wanafunzi. Mfumo huu unatoa Key Stage 3 (Darasa 7-9) na International General Certificate of Secondary Education (IGCSE) (Darasa 10-11). IGCSE, mmoja ya mitihani inayotolewa na Cambridge International Examinations, ni ya kutambulika kote duniani kama sawa na mtihani wa Uingereza wa GCSE na mtihani wa International GCE O level. IGCSE (mtaala msingi au wa kupanuliwa ) huchukuliwa katika makundi ya masomo tano: lugha, sanaa, sayansi, hisabati na ubunifu, teknolojia na ufundi. Katika siku zijazo, Key Stage 3 na IGCSE itabadilishwa na kuitwa Middle Years Programme (MYP) ya IBO.
Katika Shule ya Upili, Chuo hiki ni kinatumia Diploma ya International Baccalaureate (DP) kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 16-18. Hii ni somo la miaka miwili mfululizo ambayo huandaa wanafunzi kwa chuo kikuu. Wanafunzi wote wa DP husoma lugha, sayansi ya kijamii, na sayansi ya majaribio, hisabati na somo la sanaa. Mafanikio ya kila mwanafunzi hutahiniwa na watahiniwa huru na hupimwa kulingana na maarifa na ujuzi wa mtahiniwa.
Shule ya Aga Khan Academy, mjini Mombasa ni mojawapo ya IB Shule ya Dunia. Ilianzakufundisha Diploma ya IB mnamo Septemba 2005. IB imekuwa ya mtaala wa unaotumika katika shule za kimataifa kote duniani. Inakukubaliwa na vyuo vikuu zaidi ya 1700 kote duniani, ikiwemo Marekani, Kanada, Uingereza, bara la Ulaya, Australia na mikoa mengine mengi. IB imejulikana kuwa bora kielimu na vilevile kwa kuhamasisha huduma kwa jamii.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "The Aga Khan Academy, Mombasa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2006-11-14.
- "Brochure for the Aga Khan Academy, Mombasa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2006-10-04. Iliwekwa mnamo 2006-11-14.
- "Inauguration of the Aga Khan Academy, Mombasa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-11-11. Iliwekwa mnamo 2006-11-14.
- "The Aga Khan Schools". Iliwekwa mnamo 2006-11-14.
- "The Aga Khan Development Network". Iliwekwa mnamo 2006-11-14.