Nenda kwa yaliyomo

Adam Zuberi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adam Zuberi - Mtangazaji-Ufm

Adam Zuberi ni mtangazaji na mzalisha vipindi vya redio nchini Tanzania mwenye mapenzi na tasnia za michezo na muziki hususan wa dansi. Kwa sasa Adam ni miongoni mwa watangazaji wa redio inayomilikiwa na kampuni ya Azam, inayorusha matangazo yake kutokea Tabata, Dar Es Salaam.[1]

Kipindi chake maarufu zaidi akiwa na Ufm ni Saturday Rumba kinachorushwa kila siku ya Jumamosi usiku, kuanzia Septemba 2020. Kadhalika Adam ni mtangazaji wa vipindi vya Rumba Tosha na Sunday Rumba na ni mchangiaji kwenye vipindi vya michezo.

Adam amefanya kazi ya kupigiwa mfano na waandishi ambayo ni ya uhifadhi wa taarifa mbali mbali kuhusu muziki wa dansi pamoja na wanamuziki wa dansi. Anayafanya hayo kupitia mahojiano yake na wanamuziki na wadau wengine wa muziki na kuzihifadhi vema taarifa hizo. Yeye ni miongoni mwa Watanzania wachache waliohifadhi vema taarifa za aina hiyo pengine kuliko zilivyohifadhi taasisi ambazo zina wajibu wa kufanya hivyo.

Mifano ya wanamuziki aliofanya nao mahojiano ni pamoja na Hassan Rehani Bitchuka, Kikumbi Mwanza M'pango (King Kiki), Abdallah Gama, na wengineo.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adam Zuberi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.