Acer Predator 21x
Mandhari
(Elekezwa kutoka Acer predator 21x)
Acer Predator 21x ni tarakilishi mpakato kubwa kuliko nyingine kwa wakati wa sasa.
Tarakilishi hii ina feni tano zinazosaidia kupunguza joto wakati kifaa hiki kinapokuwa kimewashwa. Tarakilishi hii ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja na kwa ufanisi pia inaweza kuendesha michezo mbalimbali ya kielektroniki bila kukwamakwama.
Tarakilishi hii inatengenezwa nchini Uthai na mpaka sasa inapatikana sehemu nyingi ulimwenguni na kwa kuwa ina uwezo mkubwa katika kazi inauzwa bei ghali.
Tarakilishi hii haikai na chaji muda mrefu kwani inatumia umeme mwingi, hivyo muda mwingi inatakiwa kuwa imechomekwa kwenye umeme, tofauti na tarakilishi mpakato nyingine ambazo hukaa na chaji muda mrefu.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |