Abiria
Mandhari
Abiria (kutoka neno la Kiarabu عبر ˁabara kwa maana ya kuabiri, kuvuka eneo la maji) ni watu wanaosafiri kwa kupanda meli, ndege, gari, basi, pikipiki au treni.
Abiria hutumia vyombo hivyo vya usafiri kama njia ni mbali, au kama hawana usafiri wa binafsi au kama wanapendelea matumizi ya usafiri wa umma kuliko usafiri wao binafsi.
Kwa kawaida wakipanda wanalipia kiasi fulani kama nauli ili mwenye chombo hicho aweze kuwalipa dereva na wahudumu wengine pamoja na gharama za chombo chenyewe na matumizi yake.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Abiria kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |