Aaron Ramsdale
Aaron Christopher Ramsdale (alizaliwa 14 Mei 1998)[1] ni mchezaji wa soka la kulipwa wa Uingereza ambaye anacheza katika klabu ya Arsenal iliyopo katika Ligi kuu ya Uingereza(iitwayo: Premia) na timu ya taifa ya Uingereza kama golikipa.[2]
Ramsdale alianza maisha yake ya klabu kikosi cha wakubwa akichezea Sheffield United na akasajiliwa na AFC Bournemouth mwaka 2017. Baada ya kufanikiwa kucheza kwa mkopo katika klabu za Chesterfield na AFC Wimbledon, Ramsdale alicheza msimu mmoja na Bournemouth na akajiunga tena na Sheffield United kwa uhamisho wa thamani ya awali ya £18 milioni. Mnamo 2021, Ramsdale alisaini Arsenal kwa uhamisho wa rekodi ya klabu yenye thamani ya hadi £30 milioni, na kuwa kipa wao ghali zaidi.
Ramsdale ameiwakilisha Uingereza katika viwango vyote kuanzia chini ya miaka 18 hadi timu ya wakubwa, na alishinda Mashindano ya UEFA ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 19 mwaka 2017, na alikuwa katika kikosi kilichomaliza kama washindi wa£18 pili kwenye UEFA Euro 2020.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Aaron Ramsdale - Arsenal Goalkeeper - ESPN (UK)". ESPN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-13.
- ↑ "2018/19 Premier League squads confirmed". www.premierleague.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-13.