2 Pallas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Pallas kwa rangi ya Urujuanimno

2 Pallas (au Palasi; alama: ⚴) ni asteroidi ya pili iliyowahi kutambuliwa katika Mfumo wa Jua. Iligunduliwa na mtibabu na mwanaastronomia Mjerumani Heinrich Wilhelm Matthäus Olbers mnamo 28 Machi 1802.[1]

Jina la "2 Pallas" inaunganisha jina lililotolewa na Olbers, pamoja na namba ya asteroidi iliyojulikana. Jina lenyewe limanrejelea Pallas Athena aliyeabudiwa kama mungu katika dini ya Ugirki ya Kale.[2]

2 Pallas ina masi inayokadiriwa kuwa asilimia 7% ya masi yaote ya ukanda wa asteroidi. [3] Ni asteroidi kubwa ya tatu kulingana na masi yake, na ya pili kwa kuangalia kipenyo chake. Umbo lake linafanana na duaradufu yenye vipenyo kati ya km 500 na km 582.

References[hariri | hariri chanzo]

  1. JPL Small-Body Database Browser. ssd.jpl.nasa.gov (2011 [last update]). Iliwekwa mnamo March 21, 2011.
  2. (2003) Dictionary of minor planet names, Volume 1. Springer, 15. ISBN 3540002383. Retrieved on March 21, 2011. 
  3. Pitjeva, E. V. (2005). "High-Precision Ephemerides of Planets—EPM and Determination of Some Astronomical Constants" (PDF). Solar System Research 39 (3): 176. doi:10.1007/s11208-005-0033-2 . http://iau-comm4.jpl.nasa.gov/EPM2004.pdf. Retrieved 2021-02-14.