Nenda kwa yaliyomo

Željko Zečević

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Željko Zečević (alizaliwa tarehe 21 Oktoba 1963) ni kocha wa mpira wa kikapu na raia wa Serbia, ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa SLAC inayo shiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika. Pia ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Guinea.

Wasifu kama kocha

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika mji wa Belgrade, SR Serbia, SFR Yugoslavia (kwasasa Serbia), Zečević alianza kufundisha timu za vijana mwaka 1988 katika mji wa Belgrade.

Zečević alianza kufundisha nchini Italia mwaka 2000, timu ya vijana inayo fahamika kama Amatori Sniadero Udine. Katika msimu wa 2003-04, alianza majukumu na alicheza mechi yake ya kwanza mjini Potenza ya C-1.

Kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 alikuwa kocha mkuu wa Chabab Rif Al Hoceima inayo shiriki ligi ya kikapu nchini Moroko.

Wasifu kama kocha wa timu ya taifa

[hariri | hariri chanzo]

Zečević alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Misri katika mashindano ya FIBA AfroBasket mwaka 2009.

Februari mwaka 2021, Zečević alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu Guinea. Alifundisha timu hiyo kwenye mashindano ya AfroBasket mwaka 2021.