Émilie du Châtelet
Émilie du Châtelet (17 Desemba 1706 – 10 Septemba 1749) alikuwa mwanafalsafa wa asili na mwanahisabati wa nchini Ufaransa kuanzia miaka ya 1730 hadi kifo chake kutokana na matatizo wakati wa kujifungua mnamo 1749.
Mafanikio yake yalitambulika zaidi baada ya kutafsiri na kufafanua kitabu cha Isaac Newton cha Philosophiæ Naturalis Principia Mathematica chenye sheria za msingi za fizikia mnamo 1687.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Émilie du Châtelet alizaliwa tarehe 17 Desemba 1706 huko Paris, akiwa binti pekee katika familia ya watoto sita. Ndugu watatu waliishi hadi utu uzima wao: René-Alexandre (1698), Charles-Auguste (1701), na Elisabeth-Théodore (1710). Kaka yake mkubwa, René-Alexandre, alifariki mnamo 1720, na kaka aliyefuata, Charles-Auguste, alifariki mnamo 1731. Hata hivyo, kaka yake mdogo, Elisabeth-Théodore, aliishi hadi uzee wake na alifanikiwa kuwa abati na hatimaye askofu. Ndugu wengine wawili walifariki pindi wakiwa wadogo sana.[1] Du Châtelet pia alikuwa na dada wa kambo, Michelle, ambaye alizaliwa na mama yake wa kambo Anne Bellinzani, mwanamke mwenye akili ambaye alipenda elimu ya nyota.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Émilie du Châtelet kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |