Nenda kwa yaliyomo

Émile Durkheim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emile Durkheim

Émile Durkheim (15 Aprili 185815 Novemba 1917) alikuwa mtaalamu kutoka Ufaransa aliyeweka misingi ya sosholojia au sayansi ya jamii.

Aliunda mbinu za kuchunguza muundo wa jamii.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Durkheim alizaliwa na mwalimu wa Kiyahudi katika jimbo la Lorraine.

Alisoma kwenye chuo cha École Normale Supérieure.

Aliingia katika utumishi wa serikali na tangu mwaka 1902 alikuwa profesa wa ualimu kwenye chuo kikuu cha Sorbonne, Paris.

Kutokana na kazi zake taasisi yake ilibadilishwa kuwa taasisi ya kwanza ya sayansi ya jamii duniani.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Émile Durkheim kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.