Zohali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Zohari)
Rukia: urambazaji, tafuta
Zohali

Zohali (kutoka kar. "زحل" (zuhal), pia: Zohari au Sarateni kutoka Kilatini/Kiing. "Saturnus") ni sayari ya sita toka kwenye jua katika Mfumo wa jua na sayari zake. Ni sayari kubwa ya pili baada ya Mshtarii.

Inaonekana kwa macho matupu si lazima kutumia darubini. Kwa hiyo imeshajulikana tangu zamani ilitambuliwa na wataalamu wa nyakati za kale.

Inazunguka jua katika muda wa miaka ya dunia 29 na siku 166.

Uso wa Zohali haionekani kwa sababu angahewa nzito inafunika kila sehemu. Mada ya angahewa ni hasa hidrojeni. Kutokana na uzito wa angahewa shindikizo ndani yake inaongezeka sana katika vilindi vyake na kusababisha gesi za angahewa kuingia katika hali ya giligili (majimaji) inayobadilika kuwa mango (imara) hadi metali ndani zaidi.

Miezi ya Zohali[hariri | hariri chanzo]

Zohari ina miezi mingi. Miezi thelathini imepewa majina. Kati ya miezi hii Titan ni mkubwa mwenye kipenyo cha 5,150 km. Ni mwezi wa pekee unaojulikana kuwa na angahewa. Miezi ya Rhea, Dione, Tethys na Iapetus ina vipenyo kati ya 1,050 km na 1,530 km.

Bangili za Zohali[hariri | hariri chanzo]

Tabia ya pekee ya Zohali ni bangili zake. Mtu wa kwanza wa kuziona alikuwa Galileo Galilei alipolenga darubini yake kwa sayari. Lakini Galilei alishindwa kutmabua alichoona kutokana na kasoro za darubini yake. Aliandika wakati ule ya kwamba Zohali ilikuwa na "masikio". Mwaka 1655 Mholanzi Christiaan Huygens aliweza kutumia darubini kubwa zaidi akatambua masikio ya Galilei kuwa bangili inayozunguka sayari.

Siku hizi imejulikana ya kwamba bangili ni vipande vya barafu, vumbi ba mawe. Vipande vyake vina ukubwa kati ya milimita chache hadi mita kadhaa kama motokaa. Unene wa bangili ni mita mamia kadhaa.Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zohali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Mfumo wa jua na sayari zake
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Mirihi - Mshtarii - Zohali - Uranus - Neptun
Sun - Mercury - Venus - Earth (Moon) - Mars - Jupiter - Saturn - Uranus - Neptune