Yohane wa Mungu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Yohane wa Mungu (8 Machi, 1495 – 8 Machi, 1550) alikuwa mtawa nchini Hispania.
Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu.
[hariri] Maisha
Yohane wa Mungu alizaliwa nchini Ureno mwaka 1495.
Baada ya kuishi maisha ya hatari kama askari, na akitamani kutumia maisha yake yaliyokuwa yamebaki kwa kufanya matendo mema, alijitoa mhanga kabisa ili awauguze wagonjwa.
Alianzisha hospitali huko Granada nchini Hispania, na yeye pamoja na wafuasi wake wakaunda Shirika la Wauguzi la Mt. Yohane wa Mungu.
Alijulikana sana kwa upendo wake kwa wagonjwa na maskini.
Alikufa siku ya kufikisha umri wa miaka 55 kamili, tarehe 8 Machi, mwaka 1550 huko Granada.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1297-8
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yohane wa Mungu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |