Wagadugu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Wagadugu
Nchi Burkina Faso
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 2,453,496
Barabara katika kitovu cha Wagadugu karibu na uwanja wa Umoja wa Mataifa.

Wagadugu (kwa Kifaransa huandikwa Ouagadougou) ni mji mkuu wa Burkina Faso, na pia mji mkubwa kabisa wa nchi hiyo na wa mkoa wa Centre.

Mwaka 2019 idadi ya wakazi ilikuwa milioni 2,453,496, lakini mji unakua haraka.

Wagadugu iko katika jimbo la Kadiogo. Kuna ofisi za serikali na viwanda kadhaa vya nguo na vyakula.

Mji ni pia kitovu cha usafiri na mawasiliano. Kuna kiwanja cha kimataifa cha ndege na njia ya reli kwenda Abidjan (Côte d'Ivoire), halafu barabara za kwenda Lome (Togo), Bamako (Mali), Niamey (Niger), Accra (Ghana).

Wagadugu ina chuo kikuu kilichokuwa chuo cha mwanahistoria maarufu Joseph Ki-Zerbo.

Tamasha la kimataifa la filamu za Afrika (FESPACO) hufanyiwa Wagadugu.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wagadugu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.