Uranus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uranus, bangili na miezi yake
Uranus, bangili na miezi yake

Uranus ni sayari ya saba kutoka jua letu.

[hariri] Tabia

Ni sayari kubwa ya tatu ya mfumo wa jua hata kama mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 14 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake.

Ina miezi 27. Miezi mikubwa huitwa Miranda, Ariel, Umbriel, Titania na Oberon.

[hariri] Jina

Jina la sayari limeteuliwa kutokana na mungu wa Ugiriki ya Kale Uranos (Οὐρανός) aliyeaminiwa kuwa mungu wa anga. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu falaki ya zamani katika tamaduni mbalimbali haikujua sayari hiyo iliyojulikana tangu kupatikana kwa darubini tu. Imegunduliwa tarehe 13 Machi, 1781 na William Herschel.

[hariri] Tazama pia

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Uranus" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Uranus kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Mfumo wa jua na sayari zake
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Mirihi - Mshtarii - Zohali - Uranus - Neptun

Vifaa binafsi