Spaghetti
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Spaghetti ni chakula cha tambi chenye asili ya Italia Kusini. Ni tambi ya ngano yenye umbo ni nyembamba na urefu wa sentimeta 40. Hupikwa katika maji kwa dakika chache na kuliwa kwa uma baada ya kuongeza michuzi mbalimbali. Spaghetti ni aina moja ya chakula cha pasta na neno latumiwa wakati mwingine kutaja pasta kwa jumla.
Kutoka Italia chakula hiki kimeenea duniani kwa sababu hupikwa haraka ina shibe nzuri na kuna njia nyingi ya kubadilisha ladha yake. Kwa njia ya utani zimekuwa ishara kwa utamaduni wa Italia jinsi inavyoonekana katika filamu za Spaghetti Western.
[hariri] Tahadhari za kupika spaghetti
Spaghetti ni nyembamba, hivyo kuna hatari kuzipika muda mrefu mno. Kimsingi Spaghetti ni unga la ngano tu hivyo ikipikwa mno hulainika sana na kuwa karibu ugali.
Waitalia hupenda spaghetti "al dente" (ki-meno) yaani ziwe laini kiasi tu ili zisikike kidogo kwa meno wakati wa kula.
Spaghetti kama tambi zote zafaa kupikwa katika maji mengi yenye chumvi kidogo. Kwa kawaida huongezwa kidogo mafuta kwenye maji yanayosaidia zisishikane wakati wa kutoa katika sufuria.
[hariri] Michuzi
Kati ya michuzi ya kawaida ya spaghetti kuna hasa aina mbili:
- "alla Napoletana" au kufuatana na kawaida ya Napoli ni mchuzi nzito wa nyanya na viungo kama vitunguu, vitunguu saumu na majani ya kuongeza ladha. Juu yake humwagwa jibini iliyosagwa. Wengine huongeza vipande vidogo sana vya nyama iliyokaangwa pamoja na vitunguu katika supu hii.
- "alla Bolognese" au kufuatana na kawaida ya Bologna: ni mchuzi wa nyama iliyosagwa na kukaangwa katika sufuria pamoja na viungo.
Kuna aina nyingine nyingi kama vile "alle vongole" (na kome za bahari) au "alla carbonara" (mchuzi wa jibini, vipande vidogo vya nyama na yai) au "all'aglio e olio" (vitunguu saumu vilivyokaangwa kwa mafuta tu).