Petro Apselamo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Petro Apselamo (pia: Petrus Abselamus, Petrus Absalon, Petrus Balsamus na Petro wa Atroa; alifariki Kaisarea Baharini, Palestina, 11 Januari 309[1][2]) alikuwa Mkristo wa karne ya 3 aliyefia dini yake kwa kuchomwa moto wakati wa dhuluma ya kaisari Masimino baada ya kukataa mashauri mengi ya kumtaka aokoe ujana wake[3].

Mzaliwa wa Anea, karibu na Eleutheropolis (leo nchini Israeli), alijulikana kwa nguvu yake kubwa,[4] lakini pia kwa huruma na moyo wa ibada.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Januari [5][6] au 14 Oktoba. [7].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Eusebius, PG 20, 1497
  2. Louis-Sébastien Le Nain de Tillemont has stated that two different people are mentioned in the accounts. He stated that Peter Abselamus was crucified at Aulana, and that a different person, Peter Absalon, was burned at Caesarea. Cfr. Holweck, F. G. A Biographical Dictionary of the Saints. St. Louis, MO: B. Herder Book Co. 1924.
  3. Martyrologium Romanum
  4. Synaxarium Armen.
  5. Martyrologium Romanum
  6. Holweck, F. G. A Biographical Dictionary of the Saints. St. Louis, MO: B. Herder Book Co. 1924.
  7. A. Mertens,"Who was a Christian in the Holy Land?"
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.