Olimpia wa Konstantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Olimpia.

Olimpia wa Konstantinopoli (pia: Olimpia Kijana[1] ; Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 361 hivi - Nikomedia, leo nchini Uturuki, 25 Julai 408) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu ambaye, baada ya kubaki mjane bado kijana, aliishi kitawa na kusaidia maskini.

Hatimaye alifukuzwa na serikali na kufia uhamishoni kwa sababu ya kumuunga mkono askofu Yohane Krisostomo[2].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Julai[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Smith, A Dictionary of Christian Biography, Literature, Sects and Doctrines N to S Part Seven, p.73
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/81900
  3. Martyrologium Romanum

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.