Ngwini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Ngwini | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Ngwini au Pengwini ni ndege wa bahari katika familia Spheniscidae. Ndege hawa hawawezi kuruka angani lakini chini ya maji huenda kama “kupuruka”. Kwa kweli, wanaishi baharini nusu ya mwaka na wanarudi nchi kavu ili kuzaa tu. Kwa kawaida ngwini ni weupe kwa kidari na tumbo na weusi kwa mgongo (aina ya kamafleji). Huwakamata nduvi (krill), samaki, ngisi na wanyama wengine wadogo wa bahari. Hata kama kwa kawaida ngwini huhusishwa na barafu ya Antakitiki, spishi nyingi huyataga mayai yao kwa pwani za visiwa zenye miamba au ndani ya mashimo ambayo ngwini wameyachimba. Jike huyataga mayai mawili, lakini yule wa spishi za Aptenodytes hulitaga moja tu. Jike na dume huatamia mayai kwa zamu, lakini kwa kawaida kinda moja hutoka tu au kinda moja analishwa tu. Aptenodytes forsteri (Emperor Penguin) huzaa mbali na bahari juu ya barafu ya Bara la Antakitiki. Dume hutamia yai wakati jike anapotafuta chakula cha kumpa kinda.
Yaliyomo |
[hariri] Spishi za Afrika
- Aptenodytes patagonicus, Ngwini Mfalme (King Penguin)
- Eudyptes chrysocome, Ngwini Mrukaji (Rockhopper Penguin)
- Eudyptes (chrysocome) moselyi, Ngwini Mrukaji Kaskazi (Northern Rockhopper or Mosely's Penguin)
- Eudyptes chrysocome filholi, Ngwini Mrukaji Kusi (Southern Rockhopper Penguin)
- Eudyptes chrysolophus, Ngwini Mashungi-dhahabu (Macaroni Penguin)
- Pygoscelis papua, Ngwini Papua (Gentoo Penguin)
- Spheniscus demersus, Ngwini wa Afrika (African Penguin)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Aptenodytes forsteri (Emperor Penguin)
- Eudyptes chrysocome (Rockhopper Penguin)
- Eudyptes chrysocome chrysocome (Southern Rockhopper Penguin)
- Eudyptes pachyrhynchus (Fiordland Penguin)
- Eudyptes robustus (Snares Penguin)
- Eudyptes schlegeli (Royal Penguin) - labda namna ya E. chrysolophus tu
- Eudyptes sclateri (Erect-crested Penguin)
- Eudyptula albosignata (Northern Little Penguin) jina la spishi halijakubaliwa bado
- Eudyptula albosignata albosignata (White-flippered Penguin)
- Eudyptula minor (Little or Fairy Penguin)
- Megadyptes antipodes (Yellow-eyed Penguin)
- Pygoscelis adeliae (Adelie Penguin)
- Pygoscelis antarcticus (Chinstrap Penguin)
- Spheniscus humboldti (Humboldt Penguin)
- Spheniscus magellanicus (Magellan Penguin)
- Spheniscus mendiculus (Galápagos Penguin)
[hariri] Spishi za kabla ya historia
- Eudyptes sp. (Chatham Islands Penguin) (Mwisho wa Quaternary? ya Visiwa vya Chatham)
- Pygoscelis calderensis (Mwisho wa Miocene ya Bahía Inglesa, Chile)
- Pygoscelis grandis (Mwisho wa Miocene/Mwanzo wa Pliocene ya Bahía Inglesa, Chile)
- Pygoscelis tyreei (Tyree's Penguin) (Pliocene ya Nyuzilandi)
[hariri] Picha