Chile

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República de Chile
Jamhuri ya Chile
Bendera ya Chile Nembo ya Chile
Bendera Nembo
Wito la taifa: "Por la razón o la fuerza"
(Kwa akili au nguvu)
Wimbo wa taifa: Puro, Chile, es tu cielo azulado
"Safi ee Chile ni anga lako ya buluu"'
Lokeshen ya Chile
Mji mkuu Santiago de Chile1
33°26′ S 70°40′ W
Mji mkubwa nchini Santiago de Chile
Lugha rasmi Kihispania
Serikali Jamhuri
Michelle Bachelet
Uhuru
Serikali ya kwanza ya uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa

18 Septemba 1810
12 Februari 1818
25 Aprili 1844
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
756,950 km² (ya 38)
1.07%2
Idadi ya watu
 - Juni 2006 kadirio
 - 2002 sensa
 - Msongamano wa watu
 
16,432,674 (ya 60)
15,116,435
21/km² (ya 184)
Fedha Peso (CLP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
— (UTC-4)
— (UTC-3)
Intaneti TLD .cl
Kodi ya simu +56

-

1 The legislative body operates in Valparaíso
2 Includes Easter Island and Isla Sala y Gómez; does not include 1,250,000 km² of claimed territory in Antarctica


Chile ni nchi ya Amerika Kusini. Eneo lake ni kanda ndefu nyembamba kati ya safu za milima ya Andes na Bahari ya Pasifiki. Imepakana na Peru, Bolivia na Argentina.

Sehemu za Chile ni pia maeneo ya Kisiwa cha Pasaka (Rapa Nui) na visiwa vya Kisiwa cha Salas y Gómez, Visiwa vya Juan Fernández (pamoja na kisiwa cha Robinson Crusoe), visiwa vya Desventuradas, Visiwa vya Ildefonso na vya Diego Ramirez. Chile inadai ya kuwa sehemu ya bara la Antaktika ni eneo lake.

ramani ya kijiografia ya Chile
Atacama

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Chile ina urefu wa 4,200 km kufuata pwani la Pasifiki na milima ya Andes. Umbali huu ni kama kutoka Cape Town kwenda Dar es Salaam. Lakini upana wa wastani wa eneo lake ni 180 km pekee. Sehemu nyembamba ya nchi ina upana wa 90 km, sehemu pana ina 240 km.

Nje ya maeneo penye uwanja mwembamba wa pwani nchi yote ni ya milima na mabonde. Sehemu kubwa ya nchi ina safu mbili za milima:

  • Andes katika mashariki na
  • Cordillera de la Costa (safu ya pwani) katika magharibi.

Katikati ya safu hizi mbili kuna bonde la kati (Valle Central) penye makazi ya idadi kubwa ya wananchi na ardhi yenye rutba ya kilimo.

Kuelekea kusini kimo cha nchi hushuka chini hadi kufikia chini ya uwiano wa bahari. Milima ya safu ya pwani huonekana sasa kama visiwa.

Katika kaskazini ya nchi hakuna bonde kubwa la kati. Nchi inapanda juu kutoka mwambao wa bahari hadi kuwa tambarare yenye kimo cha mita 1,000 - 1,500 m inayoendelea mpaka mwanzo wa safu ya Andes.

Milima[hariri | hariri chanzo]

Andes za Chile ni kati ya milima ya juu duniani kuna vilele kadhaa juu ya 6,000m.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyana ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

Flag-map of Chile.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Chile bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.