Mwandiko wa Kiebrania
Mwandiko wa Kiebrania ni mwandiko au alfabeti ya lugha ya Kiebrania ya kale na ya kisasa, pia ya Kiaramu ya Biblia na ya Talmudi.
Kuna pia lugha nyingine za Kiyahudi kama Kiyiddish na Kiladino zilizoandikwa kwa kutumia mwandiko huu.
Herufi
[hariri | hariri chanzo]Mwandiko huu unafuata mfumo wa abjadi yaani herufi zake zinaonyesha konsonanti pekee. Kuna herufi 22 na hakuna tofauti kati ya herufi kubwa na ndogo (kama vile A-a, B-b) lakini herufi kadhaa zina umbo tofauti kama zinaandikwa katikati au mwishoni mwa neno. Alama za א ה ו י zinaweza pia kuonyesha vokali ndefu. Vinginevyo kuna nukta zinazoweza kuandikwa juu au chini ya herufi za konsonanti kwa kuonyesha vokali.
Herufi tatu za ב bet, כ kaf na פ pe zinaweza kuonyesha sauti mbili tofauti, ama kwa matamshi laini au magumu. Hapo Bet inaweza kuwa na matamshi ya B au V, Kaf kama K au Kh na Pe kama P au F. Tofauti inaweza kuonyeshwa kwa kuweka nukta katikati ya herufi kwa kutofautisha namna hizi mbili. Mfano : b בּ / v ב .
Mwelekeo wa mwandiko ni kutoka kulia kwenda kushoto, sawa na Kiarabu na kinyume cha mwandiko wetu wa Kilatini.
Alef | Bet/Vet | Gimel | Dalet | He | Waw | Zayin | Khet | Tet | Yod | Kaf |
א | ב | ג | ד | ה | ו | ז | ח | ט | י | כ |
ך | ||||||||||
Lamed | Mem | Nun | Samekh | Ayin | Pe/Fe | Tsadeh | Qof | Resh | Shin/Sin | Taw |
ל | מ | נ | ס | ע | פ | צ | ק | ר | ש | ת |
ם | ן | ף | ץ |
Historia
[hariri | hariri chanzo]Asili ya mwandiko wa Kiebrania ni alfabeti ya Kifinisia. Tangu karne ya 10 KK herufi za Kifinisia zilizobadilishwa kiasi zilitumiwa kuandika Kiebrania cha kale[1]. Mwandiko huu ulitumiwa wakati wa falme za Israeli na Yudah. Baada ya uhamisho wa Babeli Wayahudi walianza kutumia namna ya mwandiko wa Kiaramu (uliotoka pia kutoka Kifinisia).
Mwandiko huo uliendelea kutumiwa kwa kuandika Kiebrania katika karne nyingi ambazo Wayahudi waliishi ugenini nje ya nchi yao ya asili. Katika karne zile Kiebrania kilikuwa lugha ya kidini na ya kitaalamu lakini haikuwa tena lugha ya kwanza.
Katika karne ya 19 na ya 20 Kiebrania kilikuwa na aina ya ufufuko kama lugha ya kila siku katika harakati ya Uzayuni na hasa tangu kuundwa kwa nchi ya Israeli.
Herufi kama namba
[hariri | hariri chanzo]Herufi zilitumiwa pia kama namba ingawa hii si kawaida tena katika Kiebrania cha kisasa.
Herufi | Maana ya namba | Herufi | Maana ya namba | Herufi | Maana ya namba | ||
---|---|---|---|---|---|---|---|
א | 1 | י | 10 | ק | 100 | ||
ב | 2 | כ | 20 | ר | 200 | ||
ג | 3 | ל | 30 | ש | 300 | ||
ד | 4 | מ | 40 | ת | 400 | ||
ה | 5 | נ | 50 | ך | 500 | ||
ו | 6 | ס | 60 | ם | 600 | ||
ז | 7 | ע | 70 | ן | 700 | ||
ח | 8 | פ | 80 | ף | 800 | ||
ט | 9 | צ | 90 | ץ | 900 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Hoffman, Joel M. 2004. In the Beginning: A Short History of the Hebrew Language. New York: New York University Press.
- Saenz-Badillos, Angel. 1993. A History of the Hebrew Language. Cambridge, England: Cambridge University Press.
- Steinberg, David. History of the Hebrew Language.
- Hebrew Alphabet Guide Archived 19 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Hebrew alphabet, meanings, and spiritual symbolism Archived 26 Novemba 2013 at the Wayback Machine.
- How to draw letters
- Official Unicode standards document for Hebrew
- Transliterate your English name into Hebrew Letters Archived 1 Aprili 2010 at the Wayback Machine.
- Hebrew Alphabet Charts
- Interactive Hebrew Alphabet Lesson Archived 27 Aprili 2015 at the Wayback Machine.
- Mobile OCR Hebrew Dictionary
Baobonye za Kiebrania kwenye Intaneti
[hariri | hariri chanzo]- LiteType.com – Virtual & Interactive Hebrew Keyboard
- Hebrew calligraphy alphabet Model Hebrew calligraphy Alphabet
- Mikledet.com – For typing Hebrew with an English keyboard (Hebrew keyboard|Hebrew layout)
- Hebrew Writing Archived 18 Oktoba 2016 at the Wayback Machine. – Typing Hebrew and Nikud using extended English keyboard (Hebrew keyboard|Hebrew Writing layout)
- Prize Find: Oldest Hebrew Inscription Archived 29 Februari 2012 at the Wayback Machine. Biblical Archaeology Review
- alefalefalef