München
München au kufuatana na uzoefu wa Kiingereza Munich (tamka: munik) ni mji mkubwa wa tatu nchini Ujerumani baada ya Berlin na Hamburg) na mji mkuu wa jimbo la Bavaria. Iko kando la mto Isar takriban mita 500 juu ya UB.
Idadi ya wakazi ni watu 1,320,000. Rundiko la jiji pana wakazi milioni miwili na nusu.
München ni kati ya vitovu muhimu wa uchumi, utamaduni na sayansi vya Ujerumani. Klabu ya soka ya Bayern München imeshinda mara 19 kombe la kitaifa na mara tatu kombe la Ulaya.
[hariri] Historia
Jina la mji latokana na makazi ya wamonaki waliokuwa na nyumba kando la Isar iliyotajwa mara ya kwanza katika hati ya mwaka 1158. Mji ukawa soko kwenye daraja ya kuvuka mto. Baada ya kuwa makao makuu ya watawala wa Bavaria mji ulianza kukua. Mnamo mwaka 1700 ulikuwa na wakazi 24,000 pekee walioongezeka kuwa 170,000 mnamo 1871 na 840,000 mwaka 1933.
[hariri] Tazama pia
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu München kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |