Milima ya Nyihara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Milima ya Nyihara iko katika Mkoa wa Mara nchini Tanzania.

Kilele kina urefu wa mita 1,355 juu ya usawa wa bahari.

Nyihara ni pia jina la kijiji kilichopo katika kata ya Kyang'ombe, tarafa ya Suba, wilaya ya Rorya, mkoa wa Mara. Ndipo milima hiyo inapopatikana. Kijiji hicho hapo mwanzo kilikuwa kinaitwa Kyawanzagi. Upande wa kaskazini hupakana na ziwa Viktoria, upande wa kusini hupakana na kijiji cha Bitiryo, upande wa mashariki hupakana na kijiji cha Kyanyamusana, upande wa magharibi hupataka na kijiji cha Ruhu na upande wa kusini-magharibi hupakana na kijiji cha Muhundwe.

Watu wa kijiji cha Nyihara hujishughulisha na kilimo cha mihogo kwa asilimia kubwa kama zao la chakula, pia hujishughulisha na biashara, uvuvi wa samaki aina ya sangara, sato na dagaa na ufugaji wa mifugo.

Wenyeji wa kijiji cha Nyihara ni Wasimbiti wenye asili ya kabila la Wakurya.

Lugha yao halisi ni Kisimbiti (Ikisimbete).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Nyihara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.