Michelle Obama
Michelle LaVaughn Obama (jina la kuzaliwa ni Michelle LaVaughn Robinson; alizaliwa 17 Januari 1964) ni Mwanasheria wa Marekani na ndiye mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama.[1] Huyu ndiye wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwa mke wa Rais wa Marekani.
Michelle alizaliwa na kukua katika kitongoji cha South Side ya Chicago na kusoma hadi kuelekea katika Chuo Kikuu cha Princeton halafu katika Kitivo cha Sheria cha Harvard.
Baada ya kumaliza elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika kampuni ya Sidley Austin, halafu akaja kuwa mmoja kati ya wafanyakazi wa meya wa Chicago Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Chicago na Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.
Michelle Obama ni dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University. Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini Chicago South Side kuliko kuishi mjini Washington, D.C.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "Meet Michelle" Archived 3 Novemba 2008 at the Wayback Machine., biographical entry at BarackObama.com
- "Michelle Obama On Love, Family & Politics" Archived 26 Januari 2009 at the Wayback Machine., interview with Katie Couric of CBS News
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Frederick, Don. "Barack Obama, 44th president of the United States", Los Angeles Times, 4 Novemba 2008. Retrieved on 2008-11-04.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michelle Obama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Orodha ya Wake wa Marais wa Marekani | |
---|---|
M. Washington · A. Adams · M. Jefferson Randolph · D. Madison · E. Monroe · L. Adams · E. Donelson · S. Jackson · A. Van Buren · A. Harrison · J. Harrison · L. Tyler · P. Tyler · J. Tyler · S. Polk · M. Taylor · A. Fillmore · J. Pierce · H. Lane · M. Lincoln · E. Johnson · J. Grant · L. Hayes · L. Garfield · M. McElroy · R. Cleveland · F. Cleveland · C. Harrison · M. McKee · F. Cleveland · I. McKinley · Edith Roosevelt · H. Taft · Ellen Wilson · Edith Wilson · F. Harding · G. Coolidge · L. Hoover · E. Roosevelt · B. Truman · M. Eisenhower · J. Kennedy · C. Johnson · P. Nixon · B. Ford · R. Carter · N. Reagan · B. Bush · H. Clinton · L. Bush · M. Obama
|