Hillary Rodham Clinton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hillary Clinton.

Hillary Rodham Clinton (jina la kuzaliwa ni: Hillary Diane Rodham 26 Oktoba, 1947) ni Seneta kutoka katika jimbo la New York, Marekani. Ameolewa na rais wa zamani wa Marekani Bw. Bill Clinton. Wakati mumewe alivyokuwa rais, Hilary alipewa jina la Mwanamke wa Kwanza au Mke wa rais wa Marekani. Hilary pia ni mmoja kati ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu mpya wa mwaka wa 2008. Anagombea kupitia Chama cha Demokrasia (kwa Kiing. Democratic Party).

Hilary vilevile ni mwanasheria na pia alikuwa Mwanamke wa Kwanza wa Arkansas kabla ya kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani. Ameanza kufanya kazi kama Seneta mnamo tarehe 3 Januari ya mwaka wa 2001.

Hillary Clinton alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa seneta wa New York. Aliendelea kuwania tena kiti hicho cha Useneta katika uchaguzi wa mwaka 2006, ambao huo pia aliibuka mshindi, na inafikiriwa na vyombo vya habari vingi na baadhi ya wanasiasa kuwa Hilary ana nafasi kubwa ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa rais unaofanyika mwaka 2008 nchini Marekani.

Yaliyomo

[hariri] Maisha ya awali na elimu

Hillary Diane Rodham alizaliwa mjini Chicago, Illinois. Jina la babake ni Hugh Rodham, Sr., na jina la mamake ni Dorothy Emma Howell Rodham. Pia ana ndugu wa kiume wawili, mmoja ni Hugh na Tony.

Alipata elimu yake katika shule ya Maine East High School na Maine South High School. Alimaliza elimu yake ya awali kunako mwaka wa 1965, na baada ya hapo akaenda kujiandikisha katika chuo cha Wellesley karibu na mji wa Boston.

Mnamo mwaka wa 1969, Rodham alielkea katika Chuo cha Sheria, kilichokuwa kinamilikiwa na Yale. Baada ya hapo akapata digrii yake ya uwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Yale mnamo mwaka wa 1973. Kisha akawa anafanya kazi ya kujitolea katika Kutuo cha Kufundishia Watoto cha Yale, kilichokuwa kinajulikana kwa jina la Yale Child Study Center.

[hariri] Ndoa na familia

Wakati anafanya kazi kama mwanachama wa kitengo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Arkansas, akaolewa na Bill Clinton. Pia Bill Clinton nae alikuwa akifanya kazi hiyo hiyo alikyokuwa anafanya mkewe katika Chuo Kukuu hicho. Wote walifahamiana wakati wanasoma katika Chuo cha Sheria cha Yale. Kwa pamoja wamebarikiwa kupata mtoto mmoja pekee aitwaye Chelsea Clinton, amezaliwa mnamo tar. 27 Februari ya mwaka wa 1980.

[hariri] Kuwa Mwanamke wa Kwanza

Wakati alivyokuwa Mwanamke wa Kwanza, alijaribu kubadilsha mfumo wa huduma ya afya. Kuna baadhi ya watu wakawa wanapinga swala hilo kwa-kuwa mikutano mingi ya mpango huo ilikuwa ikifanyika kwa siri na sio katika hadhara. Mwishowe watu wengi wakawa hawataki badiliko lolte lile katika sekta hiyo ya huduma ya afya, hivyo swala lika feli.

Jambo lingine ambalo limetokea wakati yuko kama Mwanamke wa Kwanza ni pale jamii ilipogundua kwamba Bill Clinton alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine nje, Bi. Monica Lewinsky. Kulikuwa na mzozo mkubwa katika ndoa hiyo na Clinton alipelekwa mahakamani lakini kesi ilisitishwa kwakuwa mashtaka yenyewe hayakuwa na ukweli ndani yake.

[hariri] Useneta

Alipo amua kuwa anataka kuwa Seneta, akachaguwa kuwa kuwa Seneta wa New York japokuwa haishi huko. Baadhi wali laumu juu ya hilo. Alielkea huko na akashinda katika uchaguzi wa awali na wa pili pia, uliofanyika mwaka 2006.

Wakati ule wa vita vya Iraki vinataka kuanza, alipigia kula vita hivyo hivyo. Sasa hivi amegeuka na anataka vikosi vya Kijeshi vya Kimarekani viache kupigana huko nchini Iraki.

[hariri] Kampeni za Urais

Hillary Clinton ametoa fedha nyingi kuliko mtu yeyote yule katika uchaguzi huo mkuu wa rais wa mwaka wa 2008.

[hariri] Viungo vya nje

Orodha ya Wake wa Marais wa Marekani Seal Of The President Of The United States Of America.svg
M. Washington · A. Adams · M. Jefferson Randolph · D. Madison · E. Monroe · L. Adams · E. Donelson · S. Jackson · A. Van Buren · A. Harrison · J. Harrison · L. Tyler · P. Tyler · J. Tyler · S. Polk · M. Taylor · A. Fillmore · J. Pierce · H. Lane · M. Lincoln · E. Johnson · J. Grant · L. Hayes · L. Garfield · M. McElroy · R. Cleveland · F. Cleveland · C. Harrison · M. McKee · F. Cleveland · I. McKinley · Edith Roosevelt · H. Taft · Ellen Wilson · Edith Wilson · F. Harding · G. Coolidge · L. Hoover · E. Roosevelt · B. Truman · M. Eisenhower · J. Kennedy · C. Johnson · P. Nixon · B. Ford · R. Carter · N. Reagan · B. Bush · H. Clinton · L. Bush · M. Obama
Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine