Mamba (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mamba
Mamba wa Afrika
Mamba wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Nusungeli: Diapsida
Oda: Crocodilia (Reptilia kama mamba)
Owen, 1842
Ngazi za chini

Familia 3:

Distrubition of crocodiles

Mamba au ngwena ni spishi kubwa za reptilia za oda Crocodilia. Mamba wanaishi majini na hupatikana maeneo mengi ya kitropiki katika Afrika, Asia, Australia na Amerika. Mamba hupenda kuishi katika maji baridi kama vile maziwa, mito, ardhi tepe-tepe. Mamba hula hasa wanyama wenye uti wa mgongo kama vile samaki, reptilia na mamalia na wakati mwingine hata wale wasio na uti wa mgongo kama vile jamii ya konokono , moluski na kaasi kutegemeana na aina yao hasa. Mamba bado ni mlolongo wa viumbe wa kale na husemekana kuwa wamekadiriwa kidogo mno, tangu enzi zile za mirosana.

Inaaminika spishi za mamba zilianza katika ukoo wa wanyama waliokuwa karibu na dinosauri lakini hazikuangamizwa katika tukio lililosababisha kutoweka kwa masauri miaka milioni 65 iliyopita. Mamba wamepona na kuepuka matukio mengi sana ya kutoweka.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Mamba ni miongoni mwa wanyama wenye baiolojia ya hali ya juu tofauti na muonekano wao wa kizamani. Tofauti na Reptilia wengine, wao wana ubongo wa mbele; moyo wenye vyumba vinne, sehemu ya fumbatio ifanyayo kazi kama diaframu kwa msaada wa misuli inayotumiwa kuogelea mwendo wa majini mapaka kupumua. Muonekano wa nje kwa kiasi fulani ni ishara ya maisha yao ya majini na mwindaji. Maumbile ya mamba yana mfanya awe mwindaji hodari. Wana umbo lililochongoka linalowawezesha kuogelea vizuri (mamba hubana miguu yao kwenye pande zao wakati wakiogelea, na huongeza mwendokasi wao kwa kupunguza ukinzani wa maji. Miguu yao mifupi, japokuwa haitumiki kupiga kasia wawepo kwenye maji, lakini huwasaidia sana katika kukata kona za haraka na miondoko ya ghafla kwenye maji au kuanzisha mwendo. Mamba wanatishu ngumu, ndani na mwishoni mwa kinywa chao. Tishu hiyo huzuia maji yasipite. Tundu za pua za mamba hujifunga wakati wa kuzama majini. Ndimi za mamba haziko huru, zimeshikiliwa na tishu, na matokeo yake mamba hawawezi kutoa nje ulimi wao.

Magamba ya mamba yanaaminika kuwa na matundu yenye uwezo wa kuhisi kama ule mstari wa samaki. Matundu hayo huonekana sana kwenye taya zao za juu na chini. Uwezekano mwingine ni kuwa matundu hayo ni ya kutolea taka mwili, kwa sababu hutoa kitu kama mafuta hivi ambacho hutoa/huondosha matope. Mamba wana kasi sana katika mwendo mfupi, majini na hata nchi kavu. Sababu mamba hula kwa kumkamata adui, hivyo wamekuwa na meno ambayo yamechongoka vizuri, na misuli yenye nguvu inayowezesha taya zake kufunga kwa nguvu na kwa muda mrefu. Taya hizi kufunga kwa nguvu kubwa na mpaka sasa ndiyo taya zenye uwezo wa kubana/kung’ata kwa nguvu kuliko mnyama yeyote yule. Kani/mgandamizo wa taya za mamba ni zadi ya 340atm, ukilinganisha na 270atm ya papa na 68atm ya fisi. Hata hivyo taya za midomo ya mamba hufunguliwa kwa seti ya misuli laini na dhaifu. Hivyo basi mamba wanaweza kutumika kwa masomo au safari kwa kufunga tu taya zao kwa hata mipira laini. Mamba pia wana uwezo mdogo wa kugeuza shingo yao upande mpaka upande.

Taya la mamba na nguvu zake[hariri | hariri chanzo]

Mamba ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kung’ata kwa nguvu zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote. Kwa mfano, mamba wa maji chumvi wanaopatikana Australia, wanaweza kung’ata kwa nguvu mara tatu zaidi ya simba au simba mbarara. Pia, taya la mamba lina uwezo wa hali ya juu wa hisi. Uwezo huo unazidi ule wa ncha ya kidole cha mwanadamu. Hilo linawezekanaje ukizingatia kwamba ngozi ya mamba ina magamba? Taya la mamba limefunikwa kwa maelfu ya viungo vya hisi. Kila neva imeunganishwa na fuvu la kichwa. Mpangilio huo unalinda nyuzi za neva zilizo katika taya na kufanya sehemu fulani za taya kuwa na uwezo mkubwa wa kuhisi. Kwa sababu ya kuwa na uwezo huo, mamba huweza kutofautisha chakula na uchafu mdomoni mwake. Hilo pia linamwezesha mamba jike kubeba watoto wake kwa kutumia mdomo bila kuwaua.

Biolojia na Tabia[hariri | hariri chanzo]

Mamba ni washambulizi wa kushitukiza. Husubiri mawindo, samaki au wanyama wengine wa nchi kavu wasogee karibu na kisha kufanya shambulizi la ghafla. Wakiwa wanyama wala nyama wenye damu baridi, wana metabolizimu ya taratibu sana, hivyo wanaweza kuvumilia vipindi virefu vya vifaa. Licha ya kuonekana wataratibu sana mamba ndiyo wanyama wawindaji wa hatari sana kuliko wote katika maeneo yao, na baadhi ya spishi za mamba wameonekana hata wakiwashambulia papa. Upekee maarufu kwa mamba ni ule wa mahusiano yake na ndege aina ya kitwitwi wa Misri. Ndege huyo hounekana kuwa ana mahusiano tegemezi ya kibailojia na mamba. Kulingana na taarifa zisizoaminika, ndege hao hula wadudu wanaodhuru kinywa cha mamba, na mamba huachama mdomo wake ili kuwaacha ndege hao wasafishe mdomo wake.

Mamba wengi wakubwa humeza mawe ambayo hufanya kazi kama farumi ya kusawazisha (kubansi) maizi wake na kusaidia kwenye kusawazisha chakula, sawa na mchanga kwa ndege.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]