Dinosauri
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Dinosauri | ||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Sanamu ya Tyrannosaurus Rex
|
||||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
|
Dinosauri (Kutoka Kigiriki δεινός deinos – "ya kutisha", σαῦρος sauros "mjusi; pia: dinosari, dinosau) walikuwa kundi la reptilia wakubwa sana walioishi duniani miaka mamilioni iliyopita.
Wataalamu huamini ya kwamba dinosauri walitokea miaka milioni 230 iliyopita wakapotea ghafla mnamo miaka 65 iliyopita. Ndege hutazamiwa kuwa katika nasaba ya dinosauri.
Ujuzi kuhusu wanyama hao ni kutokana na visukuku vyao (mabaki yaliyokuwa jiwe) kama mifupa, nyayo, mayai au samadi. Visukuku vya dinosauri vimepatikana kwenye mabara yote hata Antaktika kwa sababu waliishi wakati mabara yote bado yalikuwa pamoja kama bara kubwa asilia la Pangaia.
Hadi sasa spishi 500 zimegunduliwa na idadi ya spishi zilizotambuliwa inazidi kuongezeka.
Kutokana na meno yao kumewezekana kutambua chakula chao. Wengine waliguwa wala majani, wengine wala nyama. Wakubwa sana walikula majani kama vile Apatosaurus and Brachiosaurus na hao walikuwa viumbehai wakubwa kabisa waliowahi kutembea duniani.
Wala nyama waliokimbia kwa miguu miwili ya nyuma jindi wanavyofanya watu lakini pia majusi kadhaa za leo.
Kulikuwa pia na reptilia wakubwa walioruka hewani walioitwa Pterosauri lakini kinasaba hawakuwa karibu sana na dinosauri. Wengine wakubwa waliishi baharini kama Ichthyosauri na Plesiosauri hata hao walikuwa kundi nyingine.
[hariri] Picha
Picha zifuatazo zinaonyesha kwanza visukuku vya kweli vya dinosauri halafu uchoraji au sanamu zinazonyesha jinsi gani wataalamu wanadhani mnyama alionekana
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dinosauri kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dinosauri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |