Maji ya matunda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maji ya machungwa

Maji ya matunda ni kinywaji kinachopatikana kutokana na matunda ya mimea. Kuna aina nyingi sana sawa na uwingi wa matunda yanayoliwa. Hasa matunda yenye majimaji nyingi ndani yake yanafaa kwa kuyatengeneza.

Matunda yanayopendwa kwa maji yao ni kwa mfano

na mengi mengine.

Maji ya matunda huwa ni kinywaji cha afya kwa sababu ya vitamini ndani yake. Kama tunda lina asidi nyingi kiasi ndani yake sukari huongezwa lakini matunda mengine hasa kama ni mabivu na yameiva penya jua nyingi huwa na sukari ya kutosha ndani yake.

Katika nchi nyingi maji ya matunda hutengenezwa kiwandani na kuuzwa madukani. Watu wengi wanajua kuitengeneza nyumbani pia.

WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Maji ya matunda" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Maji ya matunda kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.