Majadiliano ya mtumiaji:Rehema-zamani

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Karibu sana kwenye wikipedia ya Kiswahli! Kumbe umeshapata akaunti yako! safi. Karibu tena.

Ukihitaji ushauri soma kwanza Msaada_wa_kuanzisha_makala. Ulisema ya kwanza unapenda kuchangia habari za tiba. Labda angalia makala za jamii:Tiba na jamii:Mwili. Hapa utaona njia za kupanga muundo wa makala hizi.

Ukiwa swali lolote: Karibu utuulize!!--Kipala (majadiliano) 18:26, 18 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Mwanafunzi wa kutunga makala[hariri chanzo]

(imenakiliwa kutoka ukurasa Majadiliano ya mtumiaji:Kipala)
Karibu sana dada (au: ndugu?) Rehema! Ikiwezekana naomba uchukue hatua ya kujiandikisha na kufungua ukurasa wako. Unafika ukibonyeza "sajili akaunti" kwenye kona ya juu. Hapa unapata chaguo la kujiandikisha kwenye dirisha la "Ingia - sajili akaunti". Faida yake ni ukiingia na kufanya log-in utaona mara moja kama mtu ameandika kitu kwenye ukurasa wako; pia unapewa nafasi ya kutazama makala ulizoteua. Kuhsu "figo" nina mapendekezo kadhaa lakini sasa nina kazi nyingi kidogo siku zinazozokuja. --Kipala (majadiliano) 18:08, 18 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Nakushukuru ndugu![hariri chanzo]

Nashukuru mwenzangu! Ningefurahi kupata maelekezo zaidi toka kwako, ila chukua ile nafasi unayotaka, mimi sitaandika tena kwa siku kadhaa, masomo ya muhula hii yameanza.

Tia sahihi[hariri chanzo]

Salaam Rehema, itasaidia mawasiliano ukitumia kibonye cha kuingiza sahihi yako. Badala ya kuandika unabofya nafasi yake jinsi unavyoona kwenye picha. Salaam --Kipala (majadiliano) 20:43, 19 Januari 2009 (UTC)[jibu]


Kiswahili lugha ya elimu[hariri chanzo]

Rehema napenda kukupongeza kwa msimamo wako jinsi unavyoonekana kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Nakubali kabisa ya kwamba Kiswahili kinafaa kama lugha ya elimu. Labda unajua ya kwamba mimi ni Mjerumani. Naona tatizo hilihili katika historia ya mataifa ya Ulaya. Kote tulikuwa na lugha za kigeni kama lugha ya elimu. Maendeleo ya kijamii yalipatikana wakati nchi zilianza kutumia lugha za watu. Zamani kwetu Ulaya Kilatini ilikuwa kote lugha ya elimu. Baadaye ilikuwa katika nchi mbalimbali Kifaransa na katika nchi kadhaa pia Kijerumani. Lakini idadi ya watu waliofikiwa na elimu ya juu ilibaki ndogo mno. Baada ya kutumia lugha ya watu kwenye ngazi zote za elimu hadi chuo kikuu elimu ilipanuka sana pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kisiasa. Haya huenda sambamba. Wananchi wasipoelewa wakubwa na wasomi wanajadili nini maendeleo sharti hukwama. Lugha nyingi za Ulaya ya Mashariki zilipanushwa katika karne ya 19 tu kwa matumizi ya elimu ya kisasa- mifano ni Kibulgaria, Kicheki, Kislovakia, Kikroatia, Kislovenia, Kilithuania na mengine yaliyotazamiwa awali kama lugha za wakulima au washamba tu. Kwa hiyo usikate tamaa tujenge wikipedia hii! --Kipala (majadiliano) 21:58, 15 Februari 2009 (UTC)[jibu]