Lugha za Kisemiti
Mandhari
Lugha za Kisemiti ni kundi la lugha zinazozungumzwa na watu milioni 300 hivi katika Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Mashariki. Zinahesabiwa kama tawi la lugha za Kiafrika-Kiasia.
Lugha za Kisemiti leo
[hariri | hariri chanzo]Lugha yenye wasemaji wengi ni Kiarabu. Wasemaji wengine wengi ni wale wanaotumia lugha za Ethiopia na Eritrea halafu Israel. Lugha hai za Kisemiti ni pamoja na:
- Kiarabu ambacho kinazungumzwa kwa lahaja mbalimbali, ikiwa Kiarabu sanifu ni pia lugha rasmi katika nchi nyingi za Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati (wasemaji milioni 200-220)
- Kiamhari ambayo ni lugha rasmi ya Ethiopia (wasemaji milioni 17)
- Kitigrinya ambayo ni lugha rasmi katika Eritrea na jimbo la Tigray nchini Ethiopia. (wasemaji milioni 5)
- Kiebrania ambayo ni lugha rasmi nchini Israel (wasemaji milioni 5)
- Kiaramu kilichorudi nyuma sana lakini bado kinatumika katika Syria, Irak, Uturuki na Uajemi kwa lahaja mbalimbali (kuna takriban wasemaji 500,000 hadi milioni moja
- Kimalta ambacho ni lugha ya Kisemiti ya pekee ya Ulaya, ikiwa ni lugha rasmi nchini Malta (wasemaji laki 3)
- Lugha za Bara Arabu kusini zajadiliwa hasa katika Omani na Yemeni; ni lugha tofauti na Kiarabu chenyewe (kuna bado wasemaji 300,000)
Lugha za kihistoria
[hariri | hariri chanzo]Kuna idadi kubwa ya lugha za Kisemiti zinazojulikana kama lugha za kihistoria zisizo na wasemaji tena. Kati ya lugha hizo kuna lugha za Babeli, Ashur, Kanaan, Moabu, Finisia na kwa jumla mataifa mengi zinazotajwa katika Biblia.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Burning Issues in Afro-Asiatic Linguistics Ilihifadhiwa 16 Agosti 2020 kwenye Wayback Machine., 2012.
- Jewish Language Contact, International Journal of the Sociology of Language 226), 2014.
- Ghil'ad Zuckermann (2003), Language Contact and Lexical Enrichment in Israeli Hebrew. Palgrave Macmillan. ISBN 978-1403917232 [1].