Loisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rembrandt, Timotheo na bibi yake, 1648.

Loisi (kwa Kigiriki: Λωις, Lois) alikuwa bibi wa Timotheo, mwandamizi wa Mtume Paulo katika karne ya 1 BK.

Mwanamke Myahudi aliyeishi katika maeneo ya Uturuki kusini wa leo, aliingia pamoja na binti yake Eunike, katika Ukristo.

Wote wawili wanatajwa kwa sifa katika Barua ya pili ya Paulo kwa Timotheo 1:5, ilipoandikwa, "Nakumbuka imani yako isiyo na unafiki, aliyokuwa nayo kwanza bibi yako Loisi, halafu mama yako Eunike na sasa, nina hakika, imo ndani mwako pia."

Wataalamu wengi wanawahusisha na maneno ya 2 Tim. 3:15, ambamo Timotheo anakumbushwa "jinsi tangu utotoni alivyozoea maandiko matakatifu". [1]

Umuhimu wa ushahidi huo ni kwamba, wakati Timotheo ni pingili katika mlolongo wa Mitume katika kushirikisha mamlaka ya Yesu na Mitume wake kwa vizazi vijavyo vya maaskofu, mwenyewe alipokea kwanza imani nyumbani mwake kupitia mlolongo wa akina mama.

Mara nyingi Loisi amechukuliwa kama kielelezo cha bibi Mkristo. [2]

Wengine wanafikia hatua ya kusema hao walikuwa ndugu wa Paulo, ndiyo sababu aliwafahamu vizuri.[3]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Albert Barnes, for example, says, "The mother of Timothy was a pious Hebrewess, and regarded it as one of the duties of her religion to train her son in the careful knowledge of the word of God." Barnes, Albert. "The Second Epistle of Paul To Timothy - Chapter 3 - Verse 15". Christian Classics Ethereal Library. Iliwekwa mnamo 25 October 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Dale Evans Rogers suggests that "her example, her teachings, and her faith" were strong influences in Timothy's life. Rogers, Dale Evans. "Grandparents Can ... Lead the Way to Jesus". Christian Classics Ethereal Library. Iliwekwa mnamo 25 October 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. Ellicott's Commentary for English Readers on 2 Timothy 1, accessed 2 December 2016
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Loisi kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.