Eunike

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eunike na mtoto wake Timotheo walivyochorwa na Henry Lejeune.

Eunike (kwa Kigiriki: Ευνικη, Eunike, yaani Ushindi Mzuri) alikuwa mama wa Timotheo, mwandamizi wa Mtume Paulo katika karne ya 1 BK.

Binti wa mwanamke Myahudi Loisi, aliolewa na mwanamume wa Kigiriki aliyeishi katika maeneo ya Uturuki kusini wa leo, aliingia pamoja naye katika Ukristo.

Wote wawili wanatajwa kwa sifa katika Barua ya pili ya Paulo kwa Timotheo 1:5, ilipoandikwa, "Nakumbuka imani yako isiyo na unafiki, aliyokuwa nayo kwanza bibi yako Loisi, halafu mama yako Eunike na sasa, nina hakika, imo ndani mwako pia."

Wataalamu wengi wanamhusisha Eunike na maneno ya 2 Tim. 3:15, ambamo Timotheo anakumbushwa "jinsi tangu utotoni alivyozoea maandiko matakatifu". [1]

Umuhimu wa ushahidi huo ni kwamba, wakati Timotheo ni pingili katika mlolongo wa Mitume katika kushirikisha mamlaka ya Yesu na Mitume wake kwa vizazi vijavyo vya maaskofu, mwenyewe alipokea kwanza imani nyumbani mwake kupitia mlolongo wa akina mama.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Albert Barnes, for example, says, "The mother of Timothy was a pious Hebrewess, and regarded it as one of the duties of her religion to train her son in the careful knowledge of the word of God." Barnes, Albert. "The Second Epistle of Paul To Timothy - Chapter 3 - Verse 15". Christian Classics Ethereal Library. Iliwekwa mnamo 25 October 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eunike kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.