Nenda kwa yaliyomo

Kenya Commercial Bank

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kenya Commercial Bank
Ilipoanzishwa1896
Makao MakuuKencom House, Moi Avenue, Nairobi, Kenya Kenya
Tovutihttp://www.kcbbankgroup.com/ke/index.php
Nembo
Jengo la Kenya Commercial Bank

Kenya Commercial Bank (KCB) ni kati ya benki kubwa za Kenya. Hutoa huduma za fedha na ni miongoni mwa benki tatu kubwa za kibiashara nchini Kenya ikiwa na rasilimali ya zaidi ya dola za kimarekani bilioni 2. benki zingine mbili za kibiashara kubwa ni benki ya Barclays ya Kenya na benki ya Standard Chartered Bank ya Kenya.

Makao makuu yapo jijini Nairobi. KCB ina matawi kote nchini.

Hisa za benki ya Kenya Commercial Bank (KCB Group), ambayo ndiyo kampuni iliyozaa Kenya Commercial Bank, zimeorodheshwa kwenye soko la hisa la Nairobi Stock Exchange (NSE), kwa jina la (KCB). Hisa la kamouni hiyo zimeorodheshwa kwenye soko la hisa la Uganda Securities Exchange (USE)la nchini Uganda. Serikali inashika 26% za hisa. Katika miaka iliyopita KCB ilipoteza pesa nyingi kwa kutoa mikopo kwa watu waliokosa nia au uwezo wa kurudisha pesa.

Kampuni ya Kenya Commercial Bank

[hariri | hariri chanzo]

Benki ya Kenya Commercial Bank ni mwanachama wa Kampuni za KCB. Kampuni hizo ni pamoja na: [1] [2]

Kampuni za KCB Group ndiyo kampuni kubwa zaidi ya huduma za fedha katika Afrika Mashariki na yenye rasilimali inayokadiriwa kuwa dola za kiamrekani zaidi ya bilioni US $ 2,5. Kufikia Machi mwaka 2009, kampuni ya KCB ilikuwa imeenea zaidi na ilikuwa na matawi zaidi ya 170 nchini Kenya, Rwanda, Sudan Kusini na Tanzania yaliyotoa huduma za fedha.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya benki ya Kenya Commercial Bank (KCB) inaanzia mwaka 1896 wakati benki iliyoitangulia, Benki ya Kitaifa ya India ilipofungua tawi lake katika mji wa Mombasa. Miaka nane baadaye katika mwaka wa 1904, benki kupanuliwa huduma zake hadi katika mji wa Nairobi, mji ambao ulikuwa makao makuu ya reli ilioelekea nchini Uganda.

Mabadiliko makubwa katika historia ya benki hiyo yalitokea mwaka 1958. Benki ya Grindlays iliungana na Benki ya Taifa ya India na kuunda benki ya National and Grindlays Bank. Baada ya Kenya kupata uhuru mwaka 1963, Serikali ya Kenya ilinunua asilimia 60% ya hisa katika Benki ya National & Grindlays katika jitihada ya kuleta benki karibu na wengi wa Wakenya. Mwaka 1970, Serikali ya Kenya ilichukua asilimia 100% ya umiliki wa hisa za benki hiyo ili kuidhibiti kikamilifu benki kubwa zaya kuchukua udhibiti kamili ya benki kubwa ya kibiashara nchini Kenya. Benki ya National and Grindlays Bank ilipatiwa jina jipya la Kenya Commercial Bank. Kwa miaka mingi serikali imepunguza hisa zake katika benki ya KCB na kufikia Desemba 2008 ilikuwa na asilimia 23% ya hisa.

Mwaka 1972, kampuni ya Savings Loan (Kenya) Limited ilitwaliwa ili kushughulikia fedha za mikopo ya nyumba. Mwaka 1997, kampuni nyingine ndogo, Kenya Commercial Bank (Tanzania) Limited ilianzishwa Dar es Salaam, Tanzania kutoa huduma za benki na kukuza biashara ya kuvuka mpaka.

Katika mwezi wa Mei mwaka 2006 KCB ilipanua shughuli zake hadi Kusini mwa Sudan baada ya kupatiwa leseni na Benki ya Kusini mwa Sudan. Mnamo Novemba 2007, tawi la kwanza la KCB Uganda Limited lilifunguliwa Kampala nchini Uganda, baada ya kupewa leseni na benki ya Benki ya Uganda. Mwaka 2008, KCB ilipanua matawi yake hadi Rwanda, ambapo tawi la kwanza lilifunguliwa Kigali, Desemba 2008. Benki ndogo ilitarajiwa kufunguliwa Burundi mwaka 2009.[3][4]

Mtandao wa matawi

[hariri | hariri chanzo]

Benki ya KCB ina zaidi ya matawi 150 kote nchini kenya, yanayoifanya iwe benki yenye mtandao mkubwa zaidi katika kanda hiyo. Ndiyo benki inayomiliki mitambo ya ATM yenye rajamu yake mingi zaidi nchini kenya. Tangu mwaka 2004 matawi yote nchini Kenya yamewekwa rajamu upya kama sehemu zoezi kubwa la kuipatia benki hiyo rajamu upya. Benki ya KCB imeshirikiana na Pesa Point ili kuongeza idadi ya vituo vya mitambo ya ATM ambayo wateja wanaweza kujichukulia pesa zao.

Benki ya KCB inamiliki klabu ya michezo, ambacho kina timu zinazoshiriki ligi za Kenya za soka, raga, voliboli na mpira wa vikapu. Tazama klabu ya michezo ya benki ya Kenya Commercial Bank. Tangu mwaka 2003 benki ya Kenya Commercial Bank imekuwa ikidhamini Mashindano ya Mbio za Magari - za Mabingwa wa Afrika Mashariki (ambazo zinajumuisha Mashindano ya mbio za Magari ya Kobil ya Tanzania, Pearl of Afrika ya Uganda na Safari Rally ya Kenya) na Mabingwa wa Mashindano ya Magari ya Kitaifa ya Kenya ambayo yana jumla ya misururu 8 katika mwaka.

  1. Kampuni zanachama za KCB Group
  2. Maelezo mafupi ya KCB Group Ilihifadhiwa 23 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
  3. "Historia ya KCB". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-13. Iliwekwa mnamo 2021-01-15.
  4. KCB itafungua tawi nchini Burundi mwaka 2009

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kenya Commercial Bank kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.