John Cornforth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanakemia John Cornforth

John Warcup Cornforth (amezaliwa 7 Septemba 1917) ni mwanakemia kutoka nchi ya Australia. Pia ana uraia wa Uingereza. Hasa alichunguza athari za vimeng'enya kwa misombo ya kikaboni. Mwaka wa 1975, pamoja na Vladimir Prelog alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia. Mwaka wa 1977 alipewa cheo cha "Sir".

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Cornforth kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.