Hudihudi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hudihudi
Hudihudi wa Ulaya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Upupidae (Ndege walio na mnasaba na hudihudi)
Jenasi: Upupa
Linnaeus, 1758
Spishi: U. africana Bechstein, 1811

U. antaios Olson, 1975
U. epops Linnaeus, 1758
U. marginata Cabanis & Heine, 1860

Hudihudi ni ndege wa familia Upupidae wenye ushungi mrefu na domo refu na jembamba. Mwili una rangi ya machungwa lakini mabawa ni meusi yenye miraba myeupe na mkia pia ni mweusi na una mraba mweupe mmoja. Ndege hawa wanatokea maeneo wazi wa Afrika, Asia na Ulaya. Hutafuta chakula chini wakipenya ardhi kwa domo lao, pengine hukamata wadudu hewani. Hula wadudu hasa lakini watambaachi na vyura wadogo, mbegu na beri pia. Tago lao ni tundu mtini, katika ukuta wa nje au mwamba au ndani ya kando ya mchanga. Jike huyataga mayai 6-10.

[hariri] Spishi

[hariri] Picha

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine