Chura
| Chura | ||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chura-mafunjo (Hyperolius viridiflavus)
|
||||||||
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
|
||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||
|
Nusuoda 3: |
Chura ni mnyama wa ngeli amfibia anayeanza maisha yake ndani ya maji na baada ya kupita metamofosi anaendelea kuishi kwenye nchi kavu.
Utoto katika maji [hariri]
Maisha ya chura yanaanza kama yai lililotegwa kwenye maji pamoja na mayai maelfu. Anatoka kwa umbo la ndubwi (pia: kiluwiluwi) ambayo ni funzo ya chura anaendelea na kipindi cha kwanza cha maisha yake katika maji. Anapumua kwa yavuyavu na mwanzoni hana miguu bali mapezi kama samaki na mkia. Viluwiluwi wengi wakiwa kwenye maji wanakula majani au mwani hata kama baadaye kama chura mzima wanakula wanyama wengine.
Baada ya muda kiluwiluwi anakuza miguu minne na mapafu. Utumbo unabadilika na kujiandaa kwa chakula kipya kinachopatikana kwenye nchi kavu. Umbo linazidi kufanana na chura mzima.
Kipindi hiki cha utoto kwenye maji kinadumu kati ya wiki tatu hadi miaka miwili kutegemeana na spishi za chura. Mara nyingi ni kama wiki 10 - 15.
Chura mzima kwenye nchi kavu [hariri]
Akitoka kwenye maji chakula chake ni wanyama wengine hasa wadudu. Lakini chura wakubwa wameonekana pia kula mamalia wadogo, samaki na chura wadogo zaidi. Spishi kadhaa wana ulimu wa kunata wanashika wadudu wanaopita haraka lakini wengine wanakamata windo kwa kutumia mikono yao.
Bali na maelezo haya kuna pia spishi kadhaa wanaorudi kuishi katika maji lakini wanapumua kwa mapavu na wachache sana wanaendelea kula majani. Spishi kadhaa wanaendelea kuishi kwenye miti.
Chura wenyewe wanaliwa na ndege, samaki, nyoka na mamalia. Katika nchi kadhaa watu wanakula chura, kwa mfano Ufaransa, China na Ufilipino.
Kuna takriban spishi 5,600 za chura.
Familia za Afrika [hariri]
- Archaeobatrachia
- Alytidae, Vyura ulimi-sahani
- Mesobatrachia
- Pelobatidae, Vyura miguu-sepeto
- Pipidae, Vyura makucha
- Neobatrachia
- Arthroleptidae, Vyura-filimbi
- Brevicipitidae, Vyura kichwa-kifupi
- Bufonidae, Vyura sugu
- Heleophrynidae, Vyura pepo
- Hemisotidae, Vyura pua-sepeto
- Hylidae, Vyura-miti
- Hyperoliidae, Vyura-mafunjo
- Mantellidae, Vyura bukini
- Microhylidae, Vyura domo-jembamba
- Ranidae, Vyura sahihi
- Rhacophoridae, Vyura-povu
- Sooglossidae, Vyura wa Shelisheli
| Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chura kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chura kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |