Howard Walter Florey
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Howard Walter Florey (24 Septemba, 1898 – 21 Februari, 1968) alikuwa daktari kutoka nchi ya Australia. Hasa anajulikana kwa utafiti wake wa penisilini. Alipewa cheo cha "Sir" mwaka wa 1944. Mwaka wa 1945, pamoja na Alexander Fleming na Ernst Boris Chain alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.

