Frances Ford Seymour
Frances Ford Seymour (4 Aprili 1908 – 14 Aprili 1950) alikuwa mjamaa wa New York, labda anafahamika zaidi kama mke wa pili wa mwigizaji wa filamu bwana Henry Fonda pia mama wa waigizaji filamu Jane Fonda na Peter Fonda. Frances alikuwa akisumbulia na ugonjwa wa ukichaa na kisha akijiua mwenyewe kwa kujikata na kiwembe kooni mnamo mwaka 1950 wakati bado anatumia dawa za matumizi ya muda mrefu. Alifariki akiwa na umri wa miaka 42.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Frances alizaliwa mjini Brockville, Ontario, Kanada, alikuwa binti wa Eugene Ford Seymour na Sophie Mildred Bower. Mnamo tarehe 10 Januari ya mwaka wa 1931 aliolewa na George Tuttle Brokaw, tajiri mkubwa pia ni mtu mashuhuri kweli kweli katika jiji la New York, tajiri huyu mwanzoni alimuoa Clare Booth Luce, kwa bahati mbaya wakatalikiana.
Frances na tajiri huyo walizaa mtoto mmoja aitwae Frances Brokaw.
George Tuttle Brokaw alikuja kufariki mnamo mwaka 1936, na kumuacha mjane Frances Ford Seymour akiwa na umri wa miaka 28.
Ndoa ya pili
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 16 Septemba ya mwaka wa 1936 Frances Ford Seymour aliolewa na mwigiza filamu mashuhuri bwana Henry Fonda, katika Kanisa la Kristo liliopo mjini New York. Wanandoa hao walizaa watoto wawili, mmoja Jane Seymour Fonda na Peter Fonda.