Egwini wa Evesham

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matukio ya maisha ya mtakatifu Egwini katika dirisha la kioo cha rangi.

Egwini wa Evesham, O.S.B. (Worcester, Uingereza, karne ya 7 - Evesham, 30 Desemba 717 hivi) alikuwa mmonaki Mbenedikto kutoka Mercia (Uingereza) aliyefanywa askofu wa 3 wa jimbo la Worcester.

Alijitahidi kurekebisha maadili ya mapadri na walei na kwa ajili hiyo alipingwa sana[1].

Hatimaye alianzisha monasteri ya Evesham[2].

Anaheshimiwa tangu kale na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Desemba[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.