Delta ya Nile

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Delta la Nile)

Coordinates: 30°54′N 31°7′E / 30.900°N 31.117°E / 30.900; 31.117

NASA picha ya satelite ya delta la Mto Nile katika rangi za kubuni

Delta ya Nile (Kiarabu: دلتا النيل‎) ni delta ya mto Nile iliyopo upande wa Kaskazini mwa nchi ya Misri ambapo ndipo mto Nile unapoanza kusambaa na hatimaye kuishia katika Bahari ya Mediteranea. Delta hii ni moja kati ya delta kubwa zaidi duniani. Imeanzia upande wa Magharibi ilipo Alexandria hadi Port Said kwa upande wa Mashariki.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Delta hii inachukua kiasi cha kilometa 249 za ufukwe wa bahari ya Mediterania na pia katika eneo hili hufanyika shughuli mbalimbali za kilimo. Kuanzia upande wa Kaskazini hadi Kusini delta hii inakadiriwa kuwa na urefu wa kilometa 160. Delta hii inaanzia taratibu chini kuanzia katika mji wa Cairo.

Mto Nile na Delta

Wakati mingine delta hii, hugawanywa katika vijisehemu vya Mashariki na Mashariki. Huku mto Nile wenyewe ukigawa mikono mito miwili yaani Damietta na Rosetta. Ikiwa inatiririkia katika bahari ya Mediteranea pia huwa na majina hayohayo.

Zamani, delta hii ilikuwa na mikono mito mbalimbali, lakini mikono mito hii ilipotea kutokana na jitihada za kuzuia mafuriko, kwa kukinga na kubadilisha mwelekeo. Moja kati ya mikono mito iliyopotea ni ule wa Wadi Tumilat.

Mfereji wa Suez (Suez Canal) unatiririka kuelekea Mashariki mwa delta na kuingia katika mwambao wa Ziwa Manzala kwa upande wa Kaskazini-Mashariki wa delta. Kwa upande wa Kaskazini-Magharibi pia kuna maziwa mengine matatu ambayo ni Ziwa Burullus, Ziwa Idku na Ziwa Maryut.

Mto Nile kutoka juu unaonekana kama pembetatu. Pande za delta hii zinaonekana kumong’onyoka na baadhi ya mikono mito inaonekana kupanuka wakati ikiwa inaingia katika bahari ya Mediterania. Kutokana na kujengwa kwa bwawa la Lambo la Aswan kumepunguza kuja kwa rutuba katika maeneo ya delta na hivyo kusababisha wakulima kutumia mbolea nyingi ili kurejesha hali ya rutuba katika maeneo ya kufanyia shughuli za kilimo katika eneo la delta. Sehemu ya udongo wa juu katika eneo la delta ni karibu na hatua 70 kwenda chini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Matawi ya Delta la Mto Nile na maeneo ya jirani

Watu wamekuwa wakiishi katika eneo la delta ya mto Nile kwa miaka zaidi ya elfu kadhaa, na pia wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo cha hali ya juu. Mto Nile umekuwa ulifurika katika kipindi cha mwaka angalau mara moja, lakini hali hii imekuwa ikipungua kutokana na kutengenezwa kwa bwawa la Aswan. Kumbukumbu za siku za kale zinaonesha kuwa, Delta imekuwa na milango mito kadhaa.

Kwa upande wa Mashariki hadi magharibi, milango mito ni kama, Tanitic, Mendesian, t Phatnitic au Phatmetic[1]), pia kuna milango mito ya Sebennytic, Bolbitine, na Canopic pia hujulikana kama Herakleotic. Kwa sasa kuna milango mito miwili tu, hii ni kutokana na jitihada za kuzuia mafuriko na kuporomoka kwa pande za milango mito, milango mito hiyo ni pamoja na: Damietta uliopo kwa upande wa Mashariki, na Mlango mto wa Rosetta [2]. Mlango mto huu wa Damietta upo upande wa Magharibi wa delta.

Rosetta Stone lilipatikana katika delta ya mto Nile mwaka 1787, katika bandari ya Rosetta. Katika enzi za Farao, Delta hii ilikuwa ikijulikana kama Misri ya Chini na pia ilikuwa ikiitwa "Goshen". Pia kuna sehemu kadhaa za kihistoria katika eneo la delta. [3]

Idadi ya Watu[hariri | hariri chanzo]

Kiasi cha nusu ya wakazi wa Misri, yaani kiasi cha watu milioni 80 huishi katika eneo la delta. Kwa upande wa nje kidogo ya mji mkubwa, wastani wa msongamano wa watu ni kiasi cha watu 1,000 kwa kila kilometa mraba mbili au zaidi. Mji wa Alexandria ndio mji mkubwa kuliko yote katika eneo la delta na kukadiriwa kuwa na kiasi cha watu milioni 4. Miji mingine mikubwa katika eneo la delta ni pamoja na Shubra al Khaymah, Port Said, El-Mahalla El-Kubra, El Mansura, Tanta, na Zagazig.[4]

Wanyama na Mimea[hariri | hariri chanzo]

Whiskered tern

Katika kipindi cha mwisho wa mwaka eneo la mto Nile huwa lina mwonekano mwekundu na kuwa na maua ya lotus flowers. Upande wa chini wa eneo la Nile, yaani upande wa Kaskazini, na upande wa juu yaani upande wa Kusini, kuna mimea mbalimbali inayoota kwa wingi. Mimea inayoota kwa wingi katika eneo la Mto Nile kwa upande wa chini ni yale yanayoitwa Egyptian lotus, na kwa upande wa juu hujawa na mimea inayoitwa Cyperus papyrus au (papyrus sedge), japokuwa mimea hii haioti kwa wingi wakati huu kama ulivyokuwa hapo awali.

Zaidi ya aina elfu moja ya ndege, hupatikana katika eneo la delta, ikiwa ni pamoja na ndege aina ya little gull na whiskered tern. Pia ndege wengine wanaoishi katika eneo la delta ni pamoja na grey heron, Kentish Plover, shovelers na cormorant. Pia hupatikana katika eneo hili la delta.

Wanyama wengine wanaopatikana katika eneo la delta ya Nile ni pamoja na vyura, hua, kobe nanguchiro, lakini pia kuna mamba na viboko: wanyama hawa wawili walikuwa wameenea sana katika eneo la delta katika siku za nyuma lakini siku hizi hali haipo hivyo. Aina za samaki wanaopatikana katika eneo la delta ni pamoja na samaki wa aina ya Striped mullet.

Hali ya Hewa[hariri | hariri chanzo]

Delta ya mto Nile ina tabia za Kimediterania, ambayo huwa na sifa ya mvua kidogo, kiais cha mililita 100 hadi 200 kwa wastani wa mwaka na hata hivyo mvua hizi hunyesha wakati wa miezi ya baridi. Eneo la delta huwa na kipindi cha joto katika miezi ya Julai na Agosti kiasi cha nyuzijoto 30 °C hadi nyuzijoto 48 °C. Kipindi cha baridi huwa ba kiasi cha nyuzijoto 10° hadi 19 °C. Eneo la delta huwa na hali ya unyevunyevu katika kipindi cha miezi ya baridi. Eneo la Delta limekuwa likimong’onyoka kwa wastani wa kilometa 502 kwa mwaka{{Fact|date = Aprili 2008 na inatabiriwa kuwa eneo la delta litakuwa limeisha hadi kufikia mwaka 2550.

Ugatuzi[hariri | hariri chanzo]

Miji ya kale na ya sasa eneo la Delta[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Wilson, Ian. The Exodus Enigma (1985), page 46. London: Wiedenfeld & Nicolson.
  2. Hayes, W. 'Most Ancient Egypt', p. 87, JNES, 23 (1964), 73-114.
  3. Location of the site Archived 15 Januari 2010 at the Wayback Machine., Kafr Hassan Dawood On-Line, with map of early sites of the delta.
  4. City Population website, citing Central Agency for Public Mobilisation and Statistics Egypt (web), accessed 11 Aprili 1908.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]