Hua
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Hua | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Hua ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Columbidae. Spishi nyingine huitwa tetere, kuyu au fumvu. Wana rangi kijivu, kahawia na nyupe na spishi nyingi zina rangi pinki. Jenasi ya Streptopelia inatoka Afrika lakini spishi kadhaa zimeingia Ulaya na Asia. Hua mkufu wa Ulaya na hua madoa (Spotted Dove) wamewasilishwa katika Marekani. Hua hula mbegu, matunda, mimea na pengine wadudu. Hulijenga tago lao la vijiti kwa miti au miwamba au ardhini kati ya manyasi. Jike huyataga mayai mawili kwa kawaida.
Spishi za Afrika [hariri]
- Nesoenas duboisi, Hua wa Reunion (Réunion Pink Pigeon) - imekwisha sasa (k.y. 1700)
- Nesoenas mayeri, Hua wa Morisi (Pink Pigeon)
- Nesoenas picturata, Hua wa Madagaska (Malagasy Turtle Dove)
- Nesoenas rodericana, Hua wa Rodriges (Rodrigues Pigeon au Rodrigues Dove) imekwisha sasa (kati ya karne ya 18)
- Spilopelia senegalensis, Fumvu (Laughing Dove)
- Streptopelia capicola, Tetere Macho-meusi, Hua Koge au Hakimkulu (Ring-necked Dove)
- Streptopelia decaocto, Hua Mkufu wa Ulaya (Eurasian Collared Dove)
- Streptopelia decipiens, Kuyu (Mourning Collared au African Mourning Dove)
- Streptopelia hypopyrrha, Hua wa Adamawa (Adamawa Turtle Dove)
- Streptopelia lugens, Hua Kijivucheusi (Dusky Turtle Dove)
- Streptopelia reichenowi, Hua Mabawa-meupe (White-winged Collared Dove)
- Streptopelia risoria, Hua Mkufu wa Afrika (African Collared Dove)
- Streptopelia r. domestica, Hua wa Barbari (Barbary Dove) - inafugwa tu (umma chache za kimwitu huko Marekani; hulka ya uainisho wake ina shaka)
- Streptopelia semitorquata, Tetere macho-mekundu (Red-eyed Dove)
- Streptopelia turtur, Hua wa Ulaya (European Turtle Dove)
- Streptopelia vinacea, Tetere rangi-pinki (Vinaceous Dove)
Spishi za mabara mengine [hariri]
- Macropygia amboinensis (Slender-billed Cuckoo-dove)
- Macropygia emiliana (Ruddy Cuckoo-dove)
- Macropygia mackinlayi (Mackinlay's Cuckoo-dove)
- Macropygia magna (Bar-necked Cuckoo-dove)
- Macropygia nigrirostris (Bar-tailed Cuckoo-dove)
- Macropygia phasianella (Brown Cuckoo-dove)
- Macropygia ruficeps Little Cuckoo-dove)
- Macropygia rufipennis (Andaman Cuckoo-dove)
- Macropygia tenuirostris (Philippine Cuckoo-dove)
- Macropygia unchall (Barred Cuckoo-dove)
- Reinwardtoena browni (Pied Cuckoo-dove)
- Reinwardtoena crassirostris (Crested Cuckoo-dove)
- Reinwardtoena reinwardtii (Great Cuckoo-dove)
- Spilopelia chinensis (Spotted Dove)
- Streptopelia bitorquata (Island Collared Dove)
- Streptopelia orientalis (Oriental Turtle Dove)
- Streptopelia tranquebarica (Red Turtle Dove)
- Turacoena manadensis (White-faced Dove)
- Turacoena modesta (Black Dove)