Bustani ya wanyama
Mandhari
Bustani ya wanyama ni mahali ambapo wanyama, hasa wanyamapori wa aina mbalimbali, wanatunzwa ili watu wapate kuwatazama. Siku hizi bustani Za wanyama zimekuwa pia mahali pa kutunza spishi au aina za wanyama walioko hatarini kutokomea. Vile vile bustani za wanyama zimewekwa kwa ajili ya maonyesho[1].
Miji mingi mikubwa duniani ina bustani za wanyama[2]. Katika baadhi ya bustani hizo watu hulipa kiingilio wakitaka kuingia. Hata hivyo bustani hizo hazipokei mapato ya kutosha, hivyo hazina budi kupokea pia misaada kutoka serikali.
Umuhimu wa bustani za wanyama ni katika
- kuwapatia watu nafasi ya kuona kwa macho yao wanyama wa nchi zilizo mbali
- kuwaelimisha watu juu ya wanyama wa dunia, pia kuhusu mazingira yao
- kuwa kituo cha utafiti wa kisayansi kuhusu wanyama
- kuhifadhi na kufuga aina za wanyama hatarini kutokomea, hasa wasio na mazingira asilia tena.
Marejeɒ
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ramsi Bustani ya Wanyama Johannesburg
- [http://www.zoo.ac.za Tovuti rasmi Bustani ya Wanyama Pretoria
- Bustani ya wanyama Giza (Kairo [http://web.archive.org/20070527051946/http://www.jhbzoo.org.za/ Ilihifadhiwa 27 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.-Misri)]
- Association of Zoos and Aquariums (AZA) North American Association of Zoos and Aquariums
- Zoos Worldwide Zoos, aquariums, animal sanctuaries and wildlife parks
- World Association of Zoos and Aquariums
- Zoological Gardens keeping Asian Elephants
- AIZA
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bustani ya wanyama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |