Ansgar Mtakatifu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Ansgar (labda 8 Septemba 801 – 3 Februari 865) alikuwa askofu kutoka Ufaransa.
Ametambuliwa kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni 3 Februari.
Yaliyomo |
[hariri] Maisha
Ansgar alizaliwa Amiens (Ufaransa) mwanzoni mwa karne ya 9.
Alisoma katika monasteri huko Corbie.
Mwaka 826 alienda kuhubiri Injili nchini Denmark, ambako hakufanikisha sana, hivyo akaenda Uswidi.
Aliteuliwa kuwa Askofu wa Hamburg, upande wa kaskazini wa Ujerumani. Pia alikuwa balozi wa Papa Gregori IV katika Denmark na Uswidi.
Alivumilia magumu mengi sana katika kazi ya uenezazi Injili, lakini hakukata tamaa.
Alikufa huko Bremen (Ujerumani) mwaka 865.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1281
[hariri] Viungo vya nje
- Ansgar at Birka History of Birka
- Vita Ansgari, English translation from Medieval sourcebook
- German History Forum
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ansgar Mtakatifu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |