Anastasi wa Persia na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro mdogo katika Menologion of Basil II ukionyesha mazishi ya Mt. Anastasi.

Anastasi wa Persia na wenzake 70 (walifariki Resafa, Syria, 22 Januari 628) walikuwa Wakristo waliouawa na Wasasanidi kwa ajili ya imani yao.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 22 Januari[1].

Maisha ya Anastasi[hariri | hariri chanzo]

Anastasi alizaliwa Ray, Iran akiwa mtoto wa majusi Bau.

Akiwa askari wa mfalme Khosrau II (590–628) alishiriki kuteka Yerusalemu (Israeli) na msalaba wa Yesu (614).

Katika tukio hilo alichochewa kujua habari za Ukristo na hatimaye kuzisadiki. Alipobatizwa na Modesti wa Yerusalemu alibadilisha jina lake Magundat kuwa Anastasi kwa heshima ya ufufuko wa Yesu.

Miaka 7 baada ya kujiunga na monasteri alijisikia hamu ya kufia dini yake mpya akaenda Kaisarea Baharini, aliposhambulia makuhani wa Uzoroasta, dini yake ya zamani.

Walimtesa vikali ili arudie dini hiyo, lakini alikataa. Hapo alipelekwa kwenye mto Eufrate na kumtesa tena pamoja na kumuahidia vyeo vikubwa jeshini, lakini alizidi kukataa.

Hapo walimnyonga na kumkata kichwa mtoni baada ya wengine sabini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

  • Franklin, Carmela Vircillo. The Latin dossier of Anastasius the Persian: hagiographic translations and transformations. Pontifical Institute of Mediaeval Studies, Studies and Texts 147. Toronto, 2004.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.