Amur (mto)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Mto wa Amur | |
|---|---|
|
|
|
| Chanzo | Milima ya Khingan katika Mongolia ya Kichina. |
| Mdomo | Pasifiki |
| Nchi za beseni ya mto | Urusi, China |
| Urefu | 2,824 km 4,666 km pamoja na mto Argun |
| Kimo cha chanzo | 800 m |
| Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 11,000 m³/s |
| Eneo la beseni (km²) | 1,929,955 km² |
Mto wa Amur (Kirusi: Амур; Kichina: heilong jiang) ni mto mkubwa wa Asia ya Mashariki ambao ni mpaka kati ya Urusi na China kwa maelfu ya kilomita.
Amur ina chanzo chake penye kuungana kwa tawimito ya Argun na Shilka karibu na kijiji cha Moguhe katika jimbo la Heilongjiang. Kuanzia hapa inafuata mwendo wake kwa urefu wa 2,874 km hadi kuishia katika Bahari ya Ochotsk (Pasifiki) karibu na kisiwa kikubwa cha Sakhalin. Tawimito Argun na Shilka inaanza katika Mongolia yenyewe na Mongolia ya Kichina.
Pamoja na mwendo wa Argun urefu wa mto wote ni takriban 4,666 km hivyo mto mrefu wa nane duniani.
Amur imekuwa mpaka kati ya China na Urusi tangu mkataba kati ya nchi hizi wa tar. 27 Agosti 1689.