Asia ya Mashariki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Asia ya Mashariki ni kanda la bara la Asia linalojumuisha takriban 15% za eneo la bara lote.
Nchi zifuatazo huhesabiwa kuwa sehemu za Asia ya Mashariki:
- China (pamoja na Hong Kong na Macau)
- Jamhuri ya China (Taiwan)
- Korea Kaskazini
- Korea Kusini
- Japani
- Mongolia
Kiutamaduni nchi hizi zote zimeathiriwa na China jinsi inavyonekana katika maandishi, falsafa ya Konfutse, Ubuddha wa Mahayana na mtindo wa kula kwa kutumia vijiti.

