Mongolia ya Kichina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mongolia ya Kichina ndani ya China

Mongolia ya Kichina huitwa pia "Mongolia ya Ndani" ni eneo la kujitawala ndani ya Jamhuri ya Watu wa China iliyokuwa eneo la makabila ya Wamongolia ingawa siku hizi Wahan ni wakazi wengi. Wamongolia wenyewe mara nyingi huita eneo "Mongolia ya Kusini".

Imepakana na Jamhuri ya Mongolia, Urusi na majimbo mbalimbali ya China. Eneo lake ni milioni 1.18 km² (takriban 12% za China) linalokaliwa na watu milioni 24 (2004). Mji mkuu ni Hohhot.

Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin na Kimongolia.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mongolia ya Kichina kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.