Adriane Carr

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Adriane Carr (alizaliwa mnamo 1952) ni msomi, mwanaharakati na mwanasiasa katika chama cha Green Party nchini British Columbia na Kanada Pia ni diwani katika Halmashauri ya Jiji la Vancouver. [1] Mnamo 1983 hadi 1985 alikuwa mwanachama mwanzilishi na msemaji wa kwanza wa Chama cha Green Party nchini British Columbia. Mnamo 1993 Chama kilianzisha rasmi nafasi ya "Kiongozi". Katika uchaguzi wa mkoa mnamo 2005, alipata zaidi ya 25% ya kura kijijini kwake Powell River-Sunshine Coast. Mnamo Septemba 2006 alijiuzulu wadhifa wake alipoteuliwa na Kiongozi wa Shirikisho la Chama cha Green party, Elizabeth May, kuwa mmoja wa Manaibu wake wa Chama cha Green party nchini Kanada. Mapema mwaka 2006, Carr alikuwa mwenyekiti mwenza wa kampeni iliyofaulu kupata mshirika wake wa kisiasa na rafiki wa muda mrefu Elizabeth May kuchaguliwa kuwa Kiongozi.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Carr alizaliwa huko Vancouver na kukulia katika Bara la Chini na Kootenays. Alipata shahada ya uzamili katika jiografia ya mijini kutoka Chuo Kikuu cha British Columbia mnamo 1980 na akaendelea na taaluma ya ualimu katika Chuo cha Langara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hui, Stephen (19 November 2011). "Greens' Adriane Carr elected to Vancouver city council". Vancouver, British Columbia: The Georgia Straight. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 November 2011. Iliwekwa mnamo 20 November 2011.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adriane Carr kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.